Hata hivyo
zoezi hilo limeingiwa na dosari baada ya kundi la nyuki kutokea na
kuwashambulia wabomoaji, maaskari na mashuhuda wa tukio hilo huku dereva
akilazimishwa na wachina kuendelea na ubomoaji licha ya kung'atwa na nyuki hao.
Ni tukio linaloshangaza na kuitia doa serikali kwa jeshi la polisi lenye dhamana ya kulinda usalama na raia ambalo daima huhubiria raia utii wa sheria bila shuruti sasa linaenda kinyume hadi kuletewa F.F.U kulisimamia. Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya Karagwe hakupatikana kuzungumzia sakata hilo ambapo inadaiwa kuwa bomoabomoa hiyo itaigharimu halmashauri hiyo baadhi ya ofisi zitakazobomolewa ikiwemo ofisi za wabunge wa majimbo ya Karagwe na Kyerwa.
Picha/Habari
Na:-Hilali Alexander
Ruhundwa –Karagwe.
|
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
No comments:
Post a Comment