UJIRANI MWEMA:-Tazama Picha Jinsi Ngara Stars ilivyoifunga 2-0 Timu ya Olimpic Mukenke FC ya wilaya ya Bwambarangwe,mkoa wa Kirundo Nchini Burundi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 18, 2014

UJIRANI MWEMA:-Tazama Picha Jinsi Ngara Stars ilivyoifunga 2-0 Timu ya Olimpic Mukenke FC ya wilaya ya Bwambarangwe,mkoa wa Kirundo Nchini Burundi.


Mtotot mzalendo kutoka wilayani  Bwambarangwe mkoa wa Kirundo Nchini Burundi akionesha Upendo wake kwa kushika bendera ya Taifa la Tanzania kushoto na Burundi kulia,mikononi mwake wakati wa Mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa kati ya Timu ya Ngara Stars ya wilayani Ngara mkoani Kagera Nchini Tanzania dhidi ya wenyeji wao Olimpic Mukenke FC kwenye uwanja wa Dezayi Agosti 17,2014.


.........Wenyeji wetu Olimpic Mukenke FC kwenye uwanja wa Dezayi.........


Juu na Chini pichani ni kikosi cha  Olimpic Mukenke FC kwenye uwanja wa Dezayi wakipasha musuli kabla ya mchezo kuanza dhidi ya Ngara Stars.



Baraka Abbas akiwapa maelezo wachezaji wake wa Ngara Stars kabla ya kucheza Mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa  dhidi ya wenyeji wao Olimpic Mukenke FC kwenye uwanja wa Dezayi wilayani Bwambarangwe mkoani Kirundo nchini Burundi Agosti 17,2014.



Kikosi cha Ngara Stars kilichoanza dhidi ya  Olimpic Mukenke FC kwenye uwanja wa Dezayi.



Baada ya kuimbwa wimbo wa Taifa la Burundi na Tanzania .....Wachezaji wote walisalimiana.



Timu ya Ngara Stars ya hapa wilayani Ngara mkoani Kagera imefanikiwa kuzimisha shangwe za Mashabiki Zaidi ya Elfu waliokuwa wamejitokeza kutazama mchezo wa soka ,kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Dezayi pale ilipoichapa bao 2-0 timu ya Olimpic Mukenke FC ya wilayani Bwambarangwe,mkoa wa Kirundo nchini Burundi.

Mchezo huo wa Kimataifa wa kirafiki wenye lengo la kukuza ujirani mwema kati ya Wilaya ya Ngara na wilaya ya Bwambarangwe,umefanyika jana Agosti 17,2014 kwenye uwanja wa Dezay mjini Mukenke.

Pamoja na Mashabiki wengi waliojitokeza ,soka safi la nidhamu na ufundi,walikuwa ni Ngara Stars waliotakata na kupata ushindi wa bao 2-0 kwa goli za kipindi cha kwanza zilizofungwa na  Inosent Buninange na Ilakoze Sempiga


Mwenye kofia ni Mkuu wa wilaya ya  Bwambarangwe,mkoa wa Kirundo nchini Burundi Bw.Muhirwa Jean Marie akifatilia mchezo huo wa  Kimataifa wa kirafiki wenye lengo la kukuza ujirani mwema kati ya Wilaya ya Ngara na wilaya ya Bwambarangwe,umefanyika jana Agosti 17,2014 kwenye uwanja wa Dezay mjini Mukenke...anaefata kulia ni Bahati Kunzi Katibu wa Chama cha soka wilaya ya Ngara-NDFA na Said Salum Afisa Michezo wilaya ya Ngara.

......Bkari Salum Afisa Utamaduni  wilaya ya Ngara nae alikuwepo..........

Mwenye mtoto ni Mke wa Mkuu wa wilaya ya Bwambarangwe nae alikuwepo na kufurahishwa na mchezo huo wa soka.




Mashabiki wakitazama Mchezo huo wa Kimataifa wa kirafiki wenye lengo la kukuza ujirani mwema kati ya Wilaya ya Ngara na wilaya ya Bwambarangwe,umefanyika jana Agosti 17,2014 kwenye uwanja wa Dezay mjini Mukenke na Ngara Stars ilishinda bao 2-0.





UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad