Mahabusu Mkoani Geita June 26,2014, waliamua kuvua nguo,wakidai haki zao,uamuzi huo
uliibua tafrani mpaka Jeshi la Polisi kuingilia kati.
|
Mahabusu wakivua nguo mbele ya Mahakama.
|
Tukio hilo
lilijiri Juni 26,2014, saa 3:00 asubuhi ikiwa ni muda mfupi baada ya
kutoka mahakamani bila kesi zao kusikilizwa na kutakiwa kupanda kwenye gari la
polisi kurudishwa mahabusu.
Wakati sakata hilo likiendelea, baadhi ya watu walisikika wakisema kuna uwezekano madai ya mahabusu hao si waliyoyasema bali ni imani za kishirikina kutoka kwa waganga.
“Unaweza
kusema wanadai kusikilizwa, kumbe wanatumikia maelekezo ya waganga, wengine
wanaambiwa mkifika mahakamani vueni nguo, sasa watavuaje watu wakawaelewa, si
lazima wazue balaa la kutaka haki,” alisema mkazi mmoja wa Geita.
Iliendeelea
kudaiwa kuwa, wapo mahabusu wengi wanaofanya matendo ya kuashiria ushirikina
kwa sababu katika hali ya kawaida, si rahisi mtu timamu kuvua nguo, wengi hutumia
njia ya kugoma kula.
“Tunataka haki, tumechoka kuonewa, watu tunasingiziwa kesi za mauaji, wengine tuna kesi za wizi lakini kila siku kesi zinaahirishwa kwa madai eti hakuna ushahidi, tumefika hapa leo tunaambiwa kesi zimeahirishwa,” walisikika wakisema mahabusu hao.
Mahabusu hao
pia waligoma kuingia kwenye gari la polisi na kubaki wakiung’ang’ania
mlingoti wa bendera ya taifa iliyo mbele ya mahakama hiyo huku wakisema endapo
wangepigwa wangeing’oa bendera hiyo.
“Vaeni nguo,
mkuu wa mkoa hawezi kuja kuongea na watu mkiwa uchi hivi halafu mpande kwenye
gari twende gerezani tukazungumze,” alisema kaimu ofisa usalama wa Mkoa wa
Geita ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Mahabusu hao
walikubali kuvaa nguo lakini wakaendelea na mgomo wa kuingia kwenye gari, muda
mfupi alifika Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita, Gasper Kanyaita kuzumgumza nao
kwa niaba ya mkuu wa wilaya ndipo wakakubali kuingia kwenye gari la polisi
lenye namba za usajili PT 1166.
Stori:
MWANDISHI WETU, GEITA
No comments:
Post a Comment