UJIRANI MWEMA TANZANIA/BURUNDI:-Tazama Yaliyojiri CCM na CNDD-FDD waliposhiriki kwa pamoja Kufungua Ofisi za Chama Tawala,mkoa wa Muyinga Nchini Burundi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 20, 2014

UJIRANI MWEMA TANZANIA/BURUNDI:-Tazama Yaliyojiri CCM na CNDD-FDD waliposhiriki kwa pamoja Kufungua Ofisi za Chama Tawala,mkoa wa Muyinga Nchini Burundi.


Raia wa Burundi wametakiwa kuimarisha  umoja   na mshikamano  katika kuleta amani baina yao na nchi jirani  wakilenga  kujikwamua  kisiasa na kiuchumi.

Mwenyekiti wa   Chama cha Mapinduzi wilayani Ngara mkoani Kagera  Bw Hadso Bagege    ametoa kauli hiyo jana nchini Burundi katika ziara  ya   kujenga mahusiano baina ya CCM  na chama tawala  cha CNDD-FDD nchini Burundi.

Akihutubia Wananchi wa Mkoa wa Muyinga nchini Burundi,  Bw Bagege   amesema  utawala wa viongozi na kutawaliwa kwa wananchi katika kujileta maendeleo ni jambo la msingi  katika mshikamano na mahusiano katika kuimarisha Usalama , Amani  na Maendeleo.

Amesema  “Amani itatusaidia kufanya vikao vya ujirani mwema mara kwa mara kubaini wahalifu hatimaye kuwafikisha kwenye vyombo vya dola kwani wakiachwa wandidi kuhatarisha maisha ya Wananchi”

Aidha  Katibu wa chama hicho cha CCM,wilayani Ngara,mkoani Kagera nchini Tanzania, Bw Jacob Makune amesema kutokana na kuimarisha usalama, kutapunguza vita vya wenyewe kwa wenyewe katika mambo ya itikadi za kisiasa na ubaguzi wa kikabila.

Makune amesema kuwa kwa sasa Watanzania wana Mahusiano mema  na Raia wa Burundi  kutokana na Usalama wa kimipaka katika kufanya shughuli za kibiashara na kisiasa  huku wakibadilishana mbinu za kuimarisha ulinzi na usalama katika Maeneo yao.


Kamanda wa Jumuia  ya UVCCM Wilayani Ngara mkoani Kagera nchini Tanzania Bw.Hamimu Joseph  akimvisha skafu makamu Mwenyekiti wa chama cha CNDD-FDD nchini Burundi Balikukiye Victor   wakati wa ziara ya viongozi wa CCM nchini humo iliyofanyika jana Julai 19,2014.


Picha juu na chini ni Viongozi wa CCM wilayani Ngara mkoani Kagera wakipokea zawadi kutoka kwa viongozi wenzao wa chama cha CNDD -FDD nchi Burundi walipotembelea mkoa wa Muyinga   jana katika ziara ya kuimarisha mahusiano ya vyama hivyo  kisiasa.



Waliosimama: Mkuu wa mkoa wa Muyinga  nchini Burundi,Bw. Eldephonce Ntahonkunda  akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilayani Ngara mkoani Kagera,nchini Tanzania Bw.Hadson Bagege pamoja na viongizi wa CCM wilayani Ngara na wenzao wa chama tawala cha CNDD-FDD nchini  Burundi.  


Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Ngara,Mkoani Kagera nchini Tanzania Bw. Jacob Makune akihutunia wananchi wa Gasorwe mkoa wa Muyinga Nchini Burundi jana (Julai 19,2014) wakati wa ziara ya mahusiano ya Kisiasa nchini humo,nyuma waliosimama (nguo za Kijani) ni viongozi wa CCM akiwemo katibu mwenezi wa (Mwenye kofia rangi ya Taifa) Damiani Godald .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Ngara,Mkoani Kagera nchini Tanzania Bw. Hadson Bagege akihutunia wananchi wa Gasorwe mkoa wa Muyinga Nchini Burundi jana (Julai 19,2014) wakati wa ziara ya mahusiano ya Kisiasa nchini humo.

Picha juu na chini ni sehemu ya burudani ya ngoma za asili ya Warundi zikitumbuiza katika viwanja vya  Gasorwe mkoa wa Muyinga Nchini Burundi jana (Julai 19,2014) wakati wa Ufunguzi wa Ofisi ya Chama cha Kisiasa cha CNDD-FDD.
 

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa   Chama cha CNDD –FDD cha nchini Burundi ,Bw.Bulikukiye Victor amesema  wananchi wa Burundi wanashauriwa kujenga mahusiano mazuri na  wenzao wa Tanzania  ili kujifunza mbinu za kuendesha Siasa na Maendeleo.

Bw.Victor amesema Siasa ambazo hazina ubaguzi wa kidini, kikabila ama kidhahania haziwezi kusababisha kuwepo kwa vita na kujitokeza wakimbizi  ambao hutumia rasirimali za umoja wa mataifa katika kuwahudumia.

“Tunajifunza kutoka Tanzania  kwani siasa iliyoweka CNDD-FDD madarakani ni mbinu tulizopata tukiwa wakimbizi  katika makambi ya nchini mwenu tukiingia kwenye vijiji na kutafuta maisha” Alisema Victor.

Kiongozi huyo wa CNDD -FDD  alidai kuwa katika kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwa madarakani, viongozi wake walipata msaada  wa mawazo kwa viongozi na raia wa Tanzania  kujihadhari na ubaguzi kati ya Wahutu , Watusi na Watwa .

Ziara ya chama cha mapinduzi nchini Burundi ilifanyika baada ya kupata mwaliko kutoka chama cha CNDD-FDD kwenda kuhudhuria ufunguzi wa ofisi ya chama hicho katika wilaya ya Gasorwe nchini  humo iliyojengwa na wananchi.

Hii ndio Ofisi ya Chama Tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD iliyopo  Gasorwe mkoa wa Muyinga Nchini Burundi ,ilifunguliwa jana (Julai 19,2014)..Habari/Picha na Mwandishi wetu Shaaban Ndyamukama-Ngara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad