Makamu Mwenyekiti Uenezi CHADEMA, Kanda ya
Magharibi, Deogratius Liyunga akiwa amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma
(Maweni) baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana (Picha na Editha Karlo).
|
Na Editha Karlo-Kigoma.
WATU wasiojulikana wamemvamia na kumpiga pamoja na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali Makamu Mwenyekiti wa uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Magaharibi, Deogratius Liyunga na kupelekea kulazwa katika Hospita ya Mkoa wa Kigoma (Maweni).
Tukio hilo
limetokea jana majira ya saa tano usiku katika eneo la Mlole Manispaa ya
Kigoma Ujiji,wakati kiongozi huyo akiwa njiani kurudi nyumbani kwake akitokea
eneo la Mwanga kuangalia mechi za kombe la Dunia.
Akiongea na
mtandao huu wodini na alipolazwa juu ya tukio hilo,kiongozi huyo alisema kuwa
alibakiza hatua 25 iliaweze kuingia nyumbani kwake ghafla walitokea watu wanne,mmoja
alimvamia na kumkaba shingo huku wale wengine wakimshambulia kwa kisu,nyembe na
ubao.
Alisema
mbali ya watu hao kumpiga na kumjeruhi lakini walimpora fedha kiasi cha
shilingi 63,000 ingawa hawakufanikiwa kumpora simu yake ya mkononi iliyokuwa
mfukoni.
Baada ya
watu hao waliomvamia kuondoka alifanya mawasiliano kwa watu wake wa karibu
wakiwemo wanachama wa CHADEMA ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza Hospital
kwaajili ya matibabu.
Makamu
Mwenyekiti alisema kuwa tukio hilo lililomkuta linahusiano mkubwa na masuala ya
kisiasa kwani kabla ya tukio hilo amekuwa akipokea ujumbe mfupi wa maneno ya
vitisho kwenye simu yake ya mkononi kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa ni
wananchama wa chama kipya cha ACT.
Kamanda wa
polisi wa Mkoa wa Kigoma,Frasser Kashai alipopigiwa simu na mtandao huu
kuthibitisha juu ya tukio hilo alisema hana taarifa zozote kuhusiana na tukio
hilo.
''Mimi hiyo taarifa sijaipata ofisini kwangu bado ndo nina isikia kutoka kwako ngoja nifuatilie nitakujulisha'' alisema Kashai.
''Mimi hiyo taarifa sijaipata ofisini kwangu bado ndo nina isikia kutoka kwako ngoja nifuatilie nitakujulisha'' alisema Kashai.
No comments:
Post a Comment