KOMBE LA DUNIA 2014-BRAZILI:-Yaliyojili katika Fainali Julai 13,2014,Ujerumani Bingwa,Kiatu cha Dhahabu-James Rodriquez,Lionel Messi,Paul Pogba na Kipa Manuel Neuer wakiibuka Bora. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 14, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014-BRAZILI:-Yaliyojili katika Fainali Julai 13,2014,Ujerumani Bingwa,Kiatu cha Dhahabu-James Rodriquez,Lionel Messi,Paul Pogba na Kipa Manuel Neuer wakiibuka Bora.

Nahodha wa Ujerumani, Philipp Lahm (wa pili kulia mbele) akiwa ameshika Kombe la Dunia akishangilia na wachezaji wenzake Uwanja wa Maracana mjini Rio de Jeneiro,Jana Julai 13,2014 Nchini  Brazil baada ya kuifunga Argentina bao 1-0 na kutwaa taji hilo kwa Bao la ndani ya Dakika za Nyongeza 30 la Dakika ya 113 la Mario Gotze alietokea Benchi na kuingizwa Dakika ya 88.

 Hii ni mara ya kwanza kwa Nchi kutoka Ulaya kutwaa Kombe la Dunia huko Marekani ya Kusini lakini Mashabiki wa Brazil, ambao wamelikosa Kombe hilo Nyumbani kwao baada kutandikwa 7-1 na Germany kwenye Nusu Fainali, walishangilia ushindi wa Germany kwa vile Hasimu wao mkubwa ni Argentina.

Sasa Germany wamelibeba kombe hilo la FIFA la Dunia Mwaka 1954, 1974 ,1990 na 2014 huku -Argentina wametwaa Kombe la Dunia Mwaka 1986 na 1990.

Kocha wa Ujerumani, Joachim Low (katikati) akiinua Kombe la Dunia 2014.




Mtoa pasi ya bao, Andre Schurrle akipongezwa na mpenzi wake, Montana Yorke baada ya mechi ya Fainali ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Argentina na Ujerumani kushinda bao 1-0.

Lionel Messi alipewa Mpira wa Dhahabu kwa kuteuliwa kuwa Mchezaji Bora…Nae Kipa wa Germany, Manuel Neuer, ameteuliwa Kipa Bora na kushinda Glovu ya Dhahabu.


Licha ya Kupoteza mechi ya Fainali na kukosa Kombe la Dunia mwaka 2014, mshambuliaji wa Argentina na FC Barcelona, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Tuzo hii imekuja kama bahati ya kustaajabisha kwa watu wengi, lakini kwa kiasi kikubwa alistahili kupewa.

 Messi alionesha kiwango kikubwa katika hatua ya makundi akifunga mabao 4 katika michezo mitatu dhidi ya Bosnia, Iran na Nigeria, lakini nyota yake ilififia baada ya kushindwa kufunga katika mechi za mtoano dhidi ya Switzerland, Ubelgiji, Uholanzi na Ujerumani.

Katika mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani, Messi alipoteza nafasi moja muhimu, lakini muda mwingi alifanya jitihada za kutafuta upenyo bila mafanikio. 


Baada kumalizika Fainali ya Kombe la Dunia 2014,huko Maracana, Rio de Janeiro Nchini Brazil (Julai 13,2014) ambayo Germany waliifunga Argentina Bao 1-0 na kutwaa Kombe la Dunia, FIFA ilitangaza Tuzo za Wachezaji Bora na Straika wa Colombia, James ‘Bond’ Rodriguez kutwaa Buti ya Dhahabu.

Rodriguez, ambae Timu yake Colombia ilitolewa kwenye Robo Fainali na Brazil, alipachika Bao 6 kwenye Fainali hizo akifuatiwa na Thomas Muller wa Germany aliekuwa na Bao 5.

Lionel Messi alipewa Mpira wa Dhahabu kwa kuteuliwa kuwa Mchezaji Bora.
Nae Kipa wa Germany, Manuel Neuer, ameteuliwa Kipa Bora na kushinda Glovu ya Dhahabu.

Kwa upande wa Vijana, Mchezaji Bora ni Paul Pogba ndie alietwaa Tuzo ya Mchezaji Kijana.

WAGOMBEA MPIRA WA DHAHABU.

Argentina.

-Angel Di Maria
-Javier Mascherano
-Lionel Messi

Germany.

-Mats Hummels
-Toni Kroos
-Phillip Lahm
-Thomas Muller

Wengine.

-James Rodriguez [Colombia]
-Neymar [Brazil]
-Arjen Robben [Netherlands]

GLOVU YA DHAHABU.

- Keylor Navas [Costa Rica]
-Manuel Neuer [Germany]
-Sergio Romero[Argentina]

TUZO MCHEZAJI BORA KIJANA.

- Memphis Depay [Netherlands]
-Paul Pogba [France]
-Raphael Varane [France]

FIFA-KOMBE LA DUNIA 2014-BRAZIL.

MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014.
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Brazil 0 Netherlands 3
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014.
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2200
Germany 0 Argentina 0 [Dak 120, 1-0]
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad