Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika
Kazuramimba, Basanza na Uvinza, Wananchi hao walikataa kuuliza maswali mengi
badala yake wakitaka kuelekezwa utaratibu ili waweze kuunganishwa kwenye kesi
ya mbunge wao.
- Mimi sina swali, ninataka kujua ni utaratibu gani unaweza kufanywa ili niweze kuunganishwa katika kesi inayomkabili mbunge wetu, kama mbunge wetu ameitwa tumbili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya CCM ni dharau ya aina gani kwa sisi tuliomchagua, kwanini serikali ya CCM haijamkemea mwanasheria mkuu kutukejeli namna hii? ..alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Luvakubandi, mkazi wa Basanza.
Pamoja na mkazi huyo kuomba mwongozo huo, wazee kadhaa wa kata za
Kazuramimba na Uvinza nao walionekana kukerwa walipofika katika mikutano ya
Kafulila.
No comments:
Post a Comment