UCHAGUZI MKUU KLABU YA SIMBA JUNE 29,2014:-Evans Elieza Aveva ashinda Urais kwa kishindo-..’’Geofrey Nyange ‘Kaburu’ Makamu wake. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 30, 2014

UCHAGUZI MKUU KLABU YA SIMBA JUNE 29,2014:-Evans Elieza Aveva ashinda Urais kwa kishindo-..’’Geofrey Nyange ‘Kaburu’ Makamu wake.

Evans Elieza Aveva ameshinda Urais wa Klabu ya Simba katika Uchaguzi mkuu wa klabu hiyo June 29, 2014 chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi,Wakili,Dk Damas Ndumbaro.


Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 1043, amefuatiwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, kura 413 na mwisho Sued Nkwabi 300.


Evans Aveva amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Klabu ya soka ya Simba katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana (June 29,2014) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Aveva alipata ushindi huo wa kimbunga baada ya kupata kura 1845 na kumgaragaza mpinzani wake Andrew Tupa aliyepata kura 387 huku kura sita zikiharibika.

Katika nafasi ya Makamu wa Rais, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 1043 huku Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ akipata kura 413 na Swedy Mkwabi akipata kura 300. 

Awali, aliyekuwa mgombea Urais wa klabu hiyo, Michael Wambura alizuiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba kuingia kwenye Ukumbi.

Wambura, alienguliwa kwa kuwa amesimamishwa uanachama na baadaye kwa kukiuka taratibu za uchaguzi, alishindwa kupiga kura kutokana na uamuzi wa kumzuia kuingia ukumbini.

Kwa mujibu wa wasimamizi waliokuwa wakihakiki uhalali wa wanachama kwenye uchaguzi huo, jina la Wambura halikuwapo katika orodha ya wanachama wanaostahili kupiga kura.

Wambura kama walivyokuwa wanachama wengine, walifika katika eneo la uchaguzi kwa ajili ya kukamilisha haki hiyo ya kikatiba, lakini alionekana kushangazwa na uamuzi huo wa kuzuiwa kupiga kura.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad