Kamanda huyo
alisema kuwa wakati polisi wakielekea katika eneo la tukio, majambazi hayo
tayari yalikuwa yameshatoroka kwa kutumia pikipiki aina ya SANLG yenye namba
T460 CVQ hiyo.
Aidha
majambazi hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake na risasi
13 na simu ya mkononi aina ya TECNO huku wakiwa wamevalia makoti meusi na
helment ili kuficha sura zao zisitambulike kwa urahisi.
Jeshi la
polisi lilipata taarifa muda mfupi zilizotolewa na raia wema ambapo kamanda wa
polisi akiongoza kuwafatilia majambazi hao walifanikiwa kuwakuta katika pori
lililopo jirani na kijiji cha Ibambila wilayani Nyangh’hwale zaidi ya km 50
kutoka mjini Geita walipofanya uharifu.
Wakiwa
wanakimbizana majambazi hao walipowaona askari jambazi mmoja aliyekuwa na
silaha aliruka kwenye pikipiki na kuanza kuwashambulia askari kwa risasi
lakini dereva wa polisi alimfuata moja kwa moja na kumgonga kwa gari jambazi
huyo na kufariki hapo hapo.
Baada
ya hapo jambazi mwingine alikimbia kwa pikipiki na askari wakaanza kumfukuza
wakishirikiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyang’hwale na kufanikiwa
kumkamata na kuanza kumshambulia na alifariki wakati anakimbizwa kupelekwa
hospitali.
Taharuki
hiyo iliyokuwa imeukumba Mji wa Geita kwa saa takribani 3 kabala hawajakamatwa
majira ya saa 2 huku baadhi ya wananchi
wamelipongeza jeshi la polisi kwa kazi waliyoifanya kwa mda mfupi mara baada ya
tukio hilo huku kamanda Konyo akiendelea kuwaasa wananchi wazidi kutoa
ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha amani katika mkoa huo.
|
No comments:
Post a Comment