Jinsi Bi Rebeka alivyopigwa shoka kichwani hadi ubongo kutoka nje.
|
Bibi mmoja Mkazi wa mtaa wa Nyahanga, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,
Rebeka Sengasenga (82), ameuawa kwa kukatwa na Shoka kichwani kwa kile
kinachohisiwa kuwa ni imani za Kishirikina.
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo limetokea leo June 25,2014,majira ya saa tatu
asubuhi katika Mtaa wa Nyahanga, wilayani humo, ambapo Marehemu Rebeka alienda
nyumbani kwa mtoto wake Bundala Sengasenga alikokuwa ameitwa na mke wa Bundala
kusaidia kuanika Dengu.
Imeelezwa kuwa Merehemu Rebeka ambaye alikuwa akiishi kwa mwanae mkubwa
Stanley Sengasenga katika mtaa huo alifika kwa Bundala muda huo baada ya kuitwa
na Magreth Richard ambaye ni mke wa Bundala kwa ajili ya shughuli hiyo.
Katika maelezo yake Magreth amesema Mama mkwe wake Marehemu Rebeka
alifikia sebuleni, na kwamba wakati yeye yuko nje, alimwona mtu ambaye
hakuweza kumfahamu akitoka sebuleni hapo na kukimbia ndipo alipoangalia na
kumkuta Rebeka ameuawa.
Taarifa za awali zimedai, kabla ya tukio Magreth ambaye kwa sasa anashikiliwa
na jeshi la polisi mjini Kahama kwa mahojiano alienda nyumba ya jirani
kuazima Shoka, ambalo baadaye limekutwa kwenye shimo la maji taka nyumbani
hapo.
Shoka hilo limepatikana baada ya mbinu za kiupelelezi za Jeshi la Polisi kuagiza gari la maji taka kuyavuta maji hayo baada ya majirani kudai hawajaona mtu aliyekimbia na shoka muda huo katika mwelekeo ambao Magreth ameelekeza. |
.....Mwili wa Bi Rebeka ukiwa eneo la tukio.......
|
Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika
hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku upelelezi ukiendelea.
|
No comments:
Post a Comment