KOMBE LA DUNIA 2014:-Nigeria yawa Timu ya Kwanza kutinga 16 bora kutoka Africa Licha ya kufungwa 3-2 na Argentina. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 25, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Nigeria yawa Timu ya Kwanza kutinga 16 bora kutoka Africa Licha ya kufungwa 3-2 na Argentina.


Ahmed Musa (kulia) akishangilia na wenzake wa Nigeria baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Argentina.


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Nigeria kimefanikiwa kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 inayoendelea nchini Brazil ,June 25, 2014,usiku huu.

Nigeria wametinga hatua hiyo wakiwa na pointi 4 mbali na kupoteza mchezo wa leo dhidi ya Argentina kwa mabao 3-2. Wamefuzu katika kundi F wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Argentina.

Timu nyingine za Afrika ambazo bado zinategemewa na mashabiki ni Algeria kutoka kundi H na Ghana ya kundi G. 

Timu za Afrika zilizoaga mashindano hayo mpaka sasa ni Cameroon na Ivory Coast.

KUNDI F
TIMU P W D L F A GD PTS
Argentina 3 2 0 0 6 3 3 9
Nigeria 3 1 1 1 3 3 0 4
Bosnia 3 1 0 2 4 4 -0 3
Iran 3 0 1 2 1 4 -3 1





IRAN 1 BOSNIA 3

Bosnia-Herzegovina Leo(June 25,2014) imeichapa Iran Bao 3-1 kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi F la Fainali za Kombe la Dunia na kuisaidia Nigeria kusonga Raundi ya Pili ya Mtoano licha ya Timu hiyo ya Afrika kufungwa na Argentina.

Zote, Bosnia na Iran, zimetolewa kwenye Fainali hizi na Argentina na Nigeria ndio zinasonga Raundi ya Pili ya Mtoano kutoka Kundi F.

Bao za Bosnia zilifungwa na Edin Dzeko, Dakika ya 23, Miralem Pjanic, 59, na Avdija Vrsajevic 83 huku Iran wakifunga katika Dakika ya 82 kupitia Reza Ghoochannejhad.


KOMBE LA DUNIA
RATIBA/MATOKEO:
MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI
**Saa za Bongo.

JUMATATU, JUNI 23, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Australia 0 - 3 Spain B Arena da Baixada
1900 Netherlands 2 - 0 Chile B Arena Corinthians
2300 Croatia 1- 3 Mexico A Arena Pernambuco
2300 Cameroon 1- 4 Brazil A Nacional
JUMANNE, JUNI 24, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Italy 0- 1 Uruguay D Estadio das Dunas
1900 Costa Rica 0 - 0 England D Estadio Mineirão
2300 Japan 1 - 4 Colombia C Arena Pantanal
2300 Greece 2 - 1 Ivory Coast C Estadio Castelão
JUMATANO, JUNI 25, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Nigeria 2 - 3 Argentina F Estadio Beira-Rio
1900 Bosnia-Herzegovina 3 - 1 Iran F Arena Fonte Nova
2300 Honduras v Switzerland E Arena Amazonia
2300 Ecuador v France E Estadio do Maracanã
ALHAMISI, JUNI 26, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 United States v Germany G Arena Pernambuco
1900 Portugal v Ghana G Nacional
2300 South Korea v Belgium H Arena Corinthians
2300 Algeria v Russia H Arena da Baixada

RAUNDI YA PILI YA MTOANO 16 BORA.

JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA MECHI NA MECHI UWANJA MJI
1900 49 Brazil v Chile Mineirão Belo Horizonte
2300 50 Colombia v Uruguay Maracanã Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA MECHI NA MECHI UWANJA MJI
1900 51 Netherlands v Mexico Castelao Fortaleza
2300 52 Costa Rica v Greece Pernambuco Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA MECHI NA MECHI UWANJA MJI
1900 53 1E v Nigeria Nacional Brasilia
2300 54 1G v 2H Beira-Rio Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA MECHI NA MECHI UWANJA MJI
1900 55 Argentina v 2E Corinthians Sao Paulo
2300 56 1H v 2G Fonte Nova Salvador


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad