Naibu Katibu m kuu mpya wa CUF pia Mbunge wa viti Maalum Magdalena Sakaya
akimshukuru Mungu baada ya kunusurika katika ajali na Lori kwenye makutano ya
barabara ya Mandela na Nyerere Dar es Salaam.
|
HATIMAYE Chama cha Wananchi (CUF) kimekamilisha mchakato wa kuchagua safu
ya uongozi wa Kitaifa kwa kuwachagua wajumbe 45 wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa
na 20 kati yao wakitokea Zanzibar.
Wajumbe hao ni miongoni mwa 143 waliogombea Baraza Kuu la Uongozi kupitia
Kanda saba za Tanzania Bara na mbili za Zanzibar ambazo ni Kanda ya Unguja na
Kanda ya Pemba.
Kuchaguliwa kwa wajumbe hao kumekamilisha safu ya Uongozi wa kitaifa
ambapo Juni 25 mwaka huu, wajumbe wa mkutano mkuu walimchagua tena Prof.
Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti na Maalim Seif Sharif Hamad kuendelea kuwa
Katibu Mkuu.
Wajumbe hao pia walimchagua Juma Duni Haji kuwa Makamu Mwenyekiti
akichukua nafasi ya Machano Khamis Ali ambaye hakugombea tena.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Prof. Lipumba aliwashukuru wajumbe wa
mkutano mkuu kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu na kufanikisha uchaguzi huo
kwa amani na usalama.
Alisema hatua hiyo imedhihirisha ukomavu wa demorasia na uvumilivu ndani
ya chama hicho, na kuwataka wajumbe waliochaguliwa kuendeleza kazi ya
kukiimarisha na kukijenga chama hicho, ili kiweze kushinda katika uchaguzi mkuu
wa mwaka 2015.
Waliochaguliwa
Wajumbe 10 wanaowakilisha Baraza Kuu Kanda ya Unguja ni Salim Bimani,
Nassor Ahmed Mazrui, Fatma Abdulhabib Ferej, Zahra Ali Hamad na Shaaban Iddi
Ahmed.
Wengine ni Pavu Juma Abdallah, Abdillahi Jihadi Hassan, Hassan Jani
Massoud, Mohd Kombo Ali na Hemed Said Nassor.
Kanda ya Pemba, wajumbe 10 ni Hamad Massoud Hamad, Abubakar Khamis Bakar,
Rukia Kassim, Said Ali Mbarouk na Khalifa Mohd Issa.
Wengine ni Omar Ali Shehe, Riziki Omar Juma, Massoud Abdallah Salim,
Hijja Hassan Hijja na Najma Khalfan Juma.
Miongoni mwa wajumbe 25 wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa kutoka Bara ni
Chifu Letalosa Yemba, Lobora Petro, Fatma Omar Kalembo, Magdalena Sakaya,
Thomas Malima na Kapasha wa Kapasha.
Wengine ni Bonifasia Mapunda, Abdul Juma Kambaya, Ashura Mustapha, Karume
Jeremia, Julius Nyanja Salim Sarwan na Katani Ahmed Katani.
No comments:
Post a Comment