KOMBE LA DUNIA 2014:-Costa Rica yashinda kwa Penati 5-3 yatinga robo fainali sasa kuchukana na Uholanzi Julai 05,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 30, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Costa Rica yashinda kwa Penati 5-3 yatinga robo fainali sasa kuchukana na Uholanzi Julai 05,2014.

Timu ya Taifa ya Uholanzi imefanikiwa kuingia hatua ya robo Fainali ya Kombe la Dunia 2014,baada ya kuifunga Mexico mabao 2-1 ikitoka nyuma ya bao 1-0 jana June 29,2014 nchini Brazil.

Mchezaji wa Uholanzi  Klaas-Jan Huntelaar alifunga kwa penalti bao la ushindi dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida, baada ya Arjen Robben kuangushwa kwenye boksi  na Marquez huku Wesley Sneidjer aliifungia bao la kusawazisha kwa Uholanzi dakika ya 88 kufuatia
Giovani dos Santos kutangulia kuifungia Mexico dakika ya 48.

Nao Costa Rica wametinga Robo Fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika Historia baada kuitoa Ugiriki kwa  Penati 5-3  baada ya kutoka sare ya Bao 1-1 katika Dakika 90 huku Sokratis Papastathopoulos akaisawazishia Ugiriki kwenye Dakika za Nyongeza na mchezo kwenda Dakika za Nyongeza 30 bila kupata Mshindi.

Costa Rica ndio waliotangulia kupata Bao kupitia Bryan Ruiz aliefunga kwenye Dakika ya 52.

Kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano, Costa Rica walifunga Penati zao 4 za kwanza lakini Theofanis Gekas akakosa Penati ya 4 ya Greece na Michael Umana kupiga ya 5 kwa Costa Rica na kuwapa ushindi kwa Penati 5-3.

Costa Rica, ambao walitoka Kundi gumu la Uingereza, Italia na Uruguay, ambao wote ni Mabingwa wa zamani wa Dunia, sasa wapo Robo Fainali na Mabingwa hao wote wamebwagwa nje na watakutana na Uholanzi hapo Jumamosi Julai


Robben, akiongea na TV za Nchini kwao Holland, alisema: “Inabidi niombe radhi. Kipindi cha Kwanza nilijiangusha. Lakini ile mwishoni ni Penati.”

Arjen Robben akiruka kwenda chini na refa Mreno, akawapa penalti Uholanzi dakika za majeruhi na Robben ameomba radhi kwa kujiangusha kwenye Mechi hiyo ya Raundi ya Pili ya Mtoano ya Kombe la Dunia huko Brazil ambapo Nchi yake Uholanzi iliibwaga Mexico 2-1 na kutinga Robo Fainali lakini.

Penati hiyo ilitolewa Dakika ya 94 na kufungwa na Klaas Jan Huntelaar baada ya Refa Pedro Proenca wa Portugal kuamua Beki na Nahodha wa Mexico, Rafael Marquez, alimwangusha Robben.






KOMBE LA DUNIA 2014.
RAUNDI YA PILI YA MTOANO
**Saa za Bongo.

JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
49
Brazil 1 - 1 Chile , Penati 3-2
Mineirão
Belo Horizonte
2300
50
Colombia 2 - 0 Uruguay
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
51
Netherlands 2 - 1 Mexico
Castelao
Fortaleza
2300
52
Costa Rica 1-1 Greece,Penati 5-3
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
53
France v Nigeria
Nacional
Brasilia
2300
54
Germany v Algeria
Beira-Rio
Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
55
Argentina v Switzerland
Corinthians
Sao Paulo
2300
56
Belgium v USA
Fonte Nova
Salvador







ROBO FAINALI-IJUMAA, JULAI 4, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Mshindi 53 v Mshindi 54 [57]
ROBO FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

2300
Brazil v Colombia [58]
ROBO FAINALI
Estadio Castelão, Fortaleza

JUMAMOSI, JULAI 5, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Mshindi 55 v Mshindi 56 [59]
ROBO FAINALI
Nacional, Brasilia

2300
Uholanzi v Costa Rica 52 [60]
ROBO FAINALI
Arena Fonte Nova, Savador


NUSU FAINALI-JUMANNE, JULAI 8, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 57 v Mshindi 58 [61]
NUSU FAINALI
Estadio Mineirão, Belo Horizonte

JUMATANO, JULAI 9, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 59 Mshindi 60 [62]
NUSU FAINALI
Arena Corinthians, Sao Paulo


MSHINDI WA TATU-JUMAMOSI, JULAI 12, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Aliefungwa 61 v Aliefungwa 62
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia


FAINALI-JUMAPILI, JULAI 13, 2014.


SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2200
Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

Wachezaji wa Costa Rica wakimpongeza mwenzao, Bryan Ruis baada ya kufunga bao la kuongoza katika sare ya 1-1 na Ugiriki Kombe la Dunia hatua ya 16 Bora. Costa Rica imeenda Robo Fainali kwa ushindi wa penalti 5-3 baada ya sare hiyo ndani ya dakika 120 na sasa itamenyana na Uholanzi, ambayo mapema iliitoa Mexico kwa kuifunga mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad