KOMBE LA DUNIA 2014:-Soma Ratiba ya mtoano ya Hatua 16 bora-June 28,2014…. Wenyeji Brazil kucheza na wenzao wa Marekani ya Kusini Chile. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 27, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Soma Ratiba ya mtoano ya Hatua 16 bora-June 28,2014…. Wenyeji Brazil kucheza na wenzao wa Marekani ya Kusini Chile.

Fainali za Kombe la Dunia 2014, Nchini Brazil  zimeingia Hatua ya Mtoano na zipo Timu 16 zinazowania kutinga Robo Fainali.

Jumamosi, June 28,2014, Wenyeji Brazil watacheza na wenzao wa Marekani ya Kusini Chile huko Estadio Mineirao Jijini Belo Horizonte.

Baadae Siku hiyo hiyo, Colombia wataivaa Uruguay Uwanjani Maracana Jijini Rio de Janeiro na Uruguay watacheza bila ya Straika wao Luis Suarez, anaechezea Liverpool huko Uingereza baada Mchezaji huyo kupigwa rungu na FIFA na kufungiwa Miezi Minne kutoshiriki shughuli yeyote ya Soka pamoja na Mechi 9 za Uruguay baada kupatikana na hatia ya kumng’ata Meno Beki wa Italy, Giorgio Chiellini.

Mbali ya Timu kuwania kutinga Robo Fainali pia ipo vita binafsi ya kugombea Buti ya Dhahabu na hadi sasa Wachezaji Wanne wanafukuzana wakiwa na Bao 4 kila mmoja.

Wachezaji hao wanne ni Thomas Muller wa Germany, ambae ndie alietwaa Tuzo hiyo Fainali zilizopita Mwaka 2010 huko Afrika Kusini, Lionel Messi na Supastaa wa Brazil, Neymar.



FIFA KOMBE LA DUNIA 2014-RAUNDI YA PILI YA MTOANO

**Saa za Bongo.

JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
49
Brazil v Chile
Mineirão
Belo Horizonte
2300
50
Colombia v Uruguay
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
51
Netherlands v Mexico
Castelao
Fortaleza
2300
52
Costa Rica v Greece
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
53
France v Nigeria
Nacional
Brasilia
2300
54
Germany v Algeria
Beira-Rio
Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
55
Argentina v Switzerland
Corinthians
Sao Paulo
2300
56
Belgium v USA
Fonte Nova
Salvador

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad