KOMBE LA DUNIA 2014:-Raundi ya pili ya mtoano-BRAZIL v CHILE, HOLLAND v MEXICO huku Penati ya Ugiriki iking’oa Ivory Coast kwa bao 2-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 25, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014:-Raundi ya pili ya mtoano-BRAZIL v CHILE, HOLLAND v MEXICO huku Penati ya Ugiriki iking’oa Ivory Coast kwa bao 2-1.


Wenyeji wa Mashindano ya Kombe la Dunia 2014,Timu ya Taifa ya Brazil wameingia Raundi ya Pili ya Mtoano kwa kishindo baada ya Staa wao mkubwa Neymar kupiga Bao 2 na kuwapa ushindi wa Bao 4-1 katika Mechi ya mwisho ya Kundi A la Fainali za Kombe la Dunia na sasa Jumamosi June 28,2014 watacheza dhidi ya Chile.


Brazil wametinga Raundi ya Pili ya Mtoano na watakutana na Chile ambao walimaliza Nafasi ya Pili toka Kundi B.
  
Matokeo ya michezo mingine Kundi C la Fainali za Kombe la Dunia 2014,Penati ya dakika 90 iliyotolewa na mwamuzi baada ya mshambuliaji wa  Ugiriki Samaras kuonekana kukwatuliwa na Sio kasha kujiangusha, imeing’oa Ivory Coast kwenye Kombe la dunia na  imeipa Ugiriki bao la pili na kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Ivory Coast.

Nao England wameiaga Brazil rasmi baada ya kutoshinda hata Mechi moja ya Fainali hizo za Kombe la Dunia kwa kumaliza Mechi zao za Kundi D kwa kutoka Sare 0-0 na Costa Rica ambao kabla ya Mechi hii walikuwa tayari wameshatinga Raundi ya Pili ya Mtoano.

Kocha Roy Hodgson aliipangua Timu yake na kuwapa nafasi Wachezaji wengi ambao hawakucheza Mechi mbili za kwanza walizofungwa na Italia 2-1 na Uruguay 2-1.

Nayo Italia wametupwa nje ya Kombe la Dunia na Uruguay baada ya kufungwa Bao 1-0 huku wakicheza pungufu kufuatia Kadi Nyekundu kwa Claudio Marchisio kwenye Dakika ya 60.

Mbali ya kufungwa na kupewa Kadi Nyekundu, hasira kubwa za Italia zipo kwa Refa Marco Rodriguez wa Mexico kwa kutoona Luis Suarez akimng’ata Meno Beki wa Italia Chiellini.

Bao la ushindi la Uruguay lilifungwa kwa Kichwa na Beki Diego Godin katika Dakika ya 81.

Toka Kundi D, Costa Rica na Uruguay zimesonga Raundi ya Pili ya Mtoano .

As It Stands Tables FIFA World Cup 2014.


Group A

CountryPWDLGDPts
Brazil flagBRZ321057
Mexico flagMEX321037
Croatia flagCRO310203
Cameroon flagCMR3003-80

Group B

CountryPWDLGDPts
Netherlands flagNED330079
Chile flagCHI320126
Spain flagSPA3102-33
Australia flagAUS3003-60

Group C

CountryPWDLGDPts
Colombia flagCOL330079
Greece flagGRE3111-24
Ivory Coast flagCIV3102-13
Japan flagJPN3012-41

Group D

CountryPWDLGDPts
Costa Rica flagCRC321037
Uruguay flagURU320106
Italy flagITA3102-13
England flagENG3012-21

Group E

CountryPWDLGDPts
France flagFRA220066
Ecuador flagECU210103
Switzerland flagSWI2101-23
Honduras flagHON2002-40

Group F

CountryPWDLGDPts
Argentina flagARG220026
Nigeria flagNGA211014
Iran flagIRN2011-11
Bos-Herce flagBIH2002-20

Group G

CountryPWDLGDPts
Germany flagGER211044
USA flagUSA211014
Ghana flagGHA2011-11
Portugal flagPOR2011-41

Group H

CountryPWDLGDPts
Belgium flagBEL220026
Algeria flagALG210113
Russia flagRUS2011-11
South Korea flagKOR2011-21


KOMBE LA DUNIA 2014.
RATIBA/MATOKEO:
MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI
**Saa za Bongo.

JUMATATU, JUNI 23, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Australia 0 -3 Spain B Arena da Baixada
1900 Netherlands 2 -0 Chile B Arena Corinthians
2300 Croatia 1- 3 Mexico A Arena Pernambuco
2300 Cameroon 1- 4 Brazil A Nacional
JUMANNE, JUNI 24, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Italy 0 -1 Uruguay D Estadio das Dunas
1900 Costa Rica 0 -0 England D Estadio Mineirão
2300 Japan 1- 4 Colombia C Arena Pantanal
2300 Greece 2 -1 Ivory Coast C Estadio Castelão
JUMATANO, JUNI 25, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Nigeria v Argentina F Estadio Beira-Rio
1900 Bosnia-Herzegovina v Iran F Arena Fonte Nova
2300 Honduras v Switzerland E Arena Amazonia
2300 Ecuador v France E Estadio do Maracanã
ALHAMISI, JUNI 26, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 United States v Germany G Arena Pernambuco
1900 Portugal v Ghana G Nacional
2300 South Korea v Belgium H Arena Corinthians
2300 Algeria v Russia H Arena da Baixada

RAUNDI YA PILI YA MTOANO 16 BORA.

JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA MECHI NA
MECHI
UWANJA MJI
1900 49
Brazil v Chile
Mineirão Belo Horizonte
2300 50
Colombia v Uruguay
Maracanã Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA MECHI NA
MECHI
UWANJA MJI
1900 51
Netherlands v Mexico
Castelao Fortaleza
2300 52
Costa Rica v  Ugiriki
Pernambuco Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA MECHI NA
MECHI
UWANJA MJI
1900 53
1E v 2F
Nacional Brasilia
2300 54
1G v 2H
Beira-Rio Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA MECHI NA
MECHI
UWANJA MJI
1900 55
1F v 2E
Corinthians Sao Paulo
2300 56
1H v 2G
Fonte Nova Salvador

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad