|
Timu ya Taifa ya Uholanzi
imejiimarisha kufuzu hatua ya 16 Bora ya
mashindano ya Kombe la Dunia 2014,kufuatia ushindi wa 3-2 dhidi ya Australia
katika mchezo mgumu wa Kundi B Uwanja wa Beira-Rio mjini Porto Alegre nchini
Brazil June 18, 2014.
Ushindi huo, unaifanya timu
ya Louis van Gaal itimize ponti 6 baada ya mechi mbili na kupaa kileleni mwa
kundi hilo, ikiwa na mabao nane ya kufunga na matatu ya kufungwa.
Mabao ya Uholanzi yamefungwa
na Arjen Robben dakika ya 20, Robin Van Persie dakika ya 58 na Memphis Depay
dakika ya 68, wakati mabao ya Australia yamefungwa na Tim Cahill dakika ya 21
na Mike Jedinak dakika ya 54 kwa penalti.
Huu ni ushindi wa pili
mfululizo kwa Uholanzi ambao waliwachapa Mabingwa Watetezi Hispamia magoli 5-1
kwenye Mechi ya kwanza lakini ni kipigo cha pili mfululizo kwa Australia ambao
walichapwa 3-1 na Chile kwenye Mechi ya Kwanza.
|
KOMBE LA DUNIA 2014.
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo.
JUMATANO, JUNI 18, 2014
|
SAA
|
MECHI
|
KUNDI
|
UWANJA
|
1900
|
Australia 3 Netherlands 2
|
B
|
Estadio Beira-Rio
|
2200
|
Spain v Chile
|
B
|
Estadio do Maracanã
|
0100
|
Cameroon v Croatia
|
A
|
Arena Amazonia
|
ALHAMISI, JUNI 19, 2014
|
SAA
|
MECHI
|
KUNDI
|
UWANJA
|
1900
|
Colombia v Ivory Coast
|
C
|
Nacional
|
2200
|
Uruguay v England
|
D
|
Arena Corinthians
|
0100
|
Japan v Greece
|
C
|
Estadio das Dunas |
|
Mchezaji Van Persie akiruka
kushangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Uholanzi dhidi ya Australia
na kuwa 2-2 , wakati picha ya juu ni Robben akishangilia bao la
kwanza aliloifungia Uholanzi katika Mchezo huo June 18,2014.
|
Baadae katika Mechi ya Pili
ya Kundi B kati ya Bingwa mtetezi Hispania alifutwa matumaini ya kutetea taji
lake kwa Mwaka huu baada ya kuchapwa bao 2-0 na Chile,magoli hayo yakifungwa na Vargas
dakika ya 19′ na Aránguiz dakika 43
.
Kwa matokeo hayo sasa
Australia na Hispania basi zote imeondoshwa nje katika Fainali hizo.
Uholanzi watacheza Mechi yao
ya mwisho ya Kundi B dhidi ya Chile hapo Jumatatu June 23,2014 bila ya Nahodha
Robin van Persie ambae Leo June 18, 2014 alipata Kadi ya Njano ya Pili na hivyo
kufungiwa Mechi moja.
Nao Australia, pengine wakiwa
wanakamilisha ratiba tu, sawa na Hipsania watakaocheza nao bila ya Mkongwe wao Tim Cahill ambae nae alipata Kadi ya Njano ya Pili na hivyo
kufungiwa Mechi moja.
Group A
Group B
Group C
Group D
Group E
Group F
Group G
Group H
No comments:
Post a Comment