..........Baadhi
ya wananchi wa Biharamulo mjini wakifatilia tukio hilo...lililotokea mchana wa Jana
Mei 04,2014…..
|
Vijana
wawili wamenusurika kufa baada ya kuokolewa na Jeshi la Polisi Mjini Biharamulo
kutokana mikononi mwa wananchi wenye hasira waliokuwa wakiwapiga baada ya
kutapeli kiasi cha shili Laki 2 kutoka katika Kontena la huduma za Simu za
Vodacom na M Pesa.
Tukio hilo
limetokea Mchana wa Mei 04,2014, Mjini Biharamulo baada ya kijana aliyefahamika
kwa jina la Anold Albogust na mwenzake aliyetambulika kwa jina moja la Godfrey
kuingia katika Kontena hilo wakitaka kuweka fedha kwenye akaunt ya M
Pesa,ambapo baadae mhudumu wa kontena hilo aligundua mbinu za kitapeli kwa
vijana hao na kuomba msaada kwa Mgambo wa eneo hilo.
Mmiliki wa
Kontena hilo Bi. Zeuda Jackob ameiambia Radio kwizera kuwa huenda vijana hao ni
vibaka wazoefu kulingana na mbinu walizotumia,kwani wakati wakijariibu
kumtapeli walikuwa na Sanduku lisilokuwa na kitu kwa ndani.
Hata
hivyo,licha ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali waliofika eneo la tukio
muda mfupi, Jeshi la polisi lilifika na kuwachukua mara moja vijana hao ambao
pia walikuwa na pikipiki.
Habari Na
Mdau wetu:-Juventus Juvenary-BIHARAMULO.
No comments:
Post a Comment