![]() |
Msako wa Fisi waliovamia makazi ya Vitongoji vitatu
vya Kijiji cha Hungumalwa Kata ya Hungumarwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza,
umezua maajabu.
|
Maajabu hayo
yamehusishwa na imani za kishirikina, baada ya fisi wawili kati ya 12 waliouawa,
kukutwa wamevalishwa shanga na Rozali, kiunoni.
Msako huo
wasiku tatu ulioanza juzi (Jumapili) unahusisha mamia ya wananchi wa Kijiji
hicho na vitongoji vyake vya Mwanzabalemi, Mwanega na Mwang’ombe, wanaotumia
siraha za jadi na mbwa wapatao 50.
Kwa mujibu
wa baadhi ya wazee wa kijiji hicho ambao hawakutaka majina yao yaandikwe,
walisema kuwa makamanda wa jadi wanaoongoza msakao huo pamoja na mbwa wao, wana
kinga za kupambana na imani za kishirikina vinginevyo wasingeweza kuua fisi
wenye shanga na Rozali wanaotumiwa kishirikina.
Alisema
kuwa, kwa muda wa miaka miwili iliyopita hadi sasa, licha ya wanyama hao
kuharibu hekali moja ya matunda aina ya Tikiti Maji yaliyokuwa yamelimwa na
mwanchi mmoja, wameua ng’ombe 109, Mbuzi 135, kondoo 127 na Nguruwe 15 katika
Vitongoji hivyo.
“Njooni
muone maajabu haya.” Alisema Malando na kufafanua “Jana (juzi Jumapili)
wananchi walifanikiwa kuua fisi kumi wawili kati yao wakiwa na maajabu. Mmoja
aliukuwa na Rozali kiunoni na mwingine akiwa na shanga kiunoni huku uume wake
ukiwa umetahiriwa kama binaadam.”
Alisema fisi
waliokutwa na vitu hivyo kiunoni, kwa imani za kabila la Kisukuma, wanadaiwa
kumilikiwa na baadhi ya watu wenye imani za kishirikina na kwamba, waliuawa
majira ya saa 8 hadi saa 10 mchana kwenye eneo la mlima wa Mwanzabalemi.
Alifafanua
kuwa, fisi kumi waliuawa (jumapili) siku ya kwanza ya msako huo na wengine
wawili waliuawa jana asubuhi na kwamba maeneo ya milima ya Mwanangi katika
Kijiji cha Buyobo na Kitongoji cha Mwanzabalemi yanasadikiwa kuwa na fisi wengi
zaidi.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Mwang’ombe Joseph Kisena alisema hadi kufikia leo (siku ya
tatu ya msako huo) watakuwa wameua fisi wengi zaidi kutokana na ushirikiano
mzuri wa Vitongoji hivyo vinavyotumia mbwa 50 na siraha mbalimbali za jadi
ikiwemo mikuki, mapanga na marungu.
Kisena
alisema, pamoja na maajabu ya fisi kuvaa shanga na Rozali kiunoni ambayo
wamejionea na kuzua imani za ushirikina kwa baadhi ya wananchi, hawatarudi
nyuma, hadi walitokomeze kundi la wanyama hao ambalo ni tishio kwa wananchi na
mifugo wao.
No comments:
Post a Comment