|
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera ,Bw.Lambris Kipuyo akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na Mkuu wa wilaya ya Bukoba Manispaa,Bi.Zipora Pangani katika eneo la Kagondo ambapo Mwenge huo wa Uhuru ukiwa wilayani Muleba Mei 03,2014,Umezindua na kufungua miradi mitano yenye thamani ya Sh Milioni305,970,235
kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wilayani humo..Picha zote Na:-Shabani Ndyamukama-Muleba.
|
|
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2014 Kitaifa wakiimba na kucheza pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kamachumu,wilayani Muleba mkoani Kagera Mei 03,2014 ambapo Mwenge huo ulikesha kabla ya kesho yake Mei 04,2014 kukabidhiwa wilayani Bukoba Vijijini kuendelea na Mbio zake.
|
|
Kiongozi wa
mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 ,Kitaifa Bi.Rachel
Steven Kassanda akihutubia Wananchi wa Kijiji cha Kabale wilayani Muleba mkoani
Kagera na kuwataka kufuata kanuni bora za Afya pamoja na matumizi sahihi ya vyandarua ili kujikinga na ugonjwa wa maralia ambao
unapunguza nguvu kazi ya taifa kwa kusababisha vifo vya watoto na wanawake wajawazito.
|
|
Picha juu na chini ni Kiongozi wa
mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 ,Kitaifa Bi.Rachel
Steven Kassanda akigawa Vyandarua vyenye Viatilifu kwa Watoto wadogo chini ya
miaka mitano na akina Mama wajawazito katika Kijiji cha Kabale wilayani Muleba mkoani Kagera wakati
akifungua zahanati ya kijiji hicho iliyojengwa kwa thamani ya Sh.73,813,535/-
|
|
Wafanya biashara wa Ng’ombe wakiingiza mifugo kwenye
Mnada wa Mifugo wa Mubunda wilayani Muleba mkoani Kagera uliofunguliwa na
Mwenge wa Uhuru 2014,ukijengwa kwa thamani ya Sh.Milioni 40, na umeelezwa kuwa
utawanufaisha wananchi kutoka wilaya za Muleba, Bukoba vijijini na Karagwe huku
ukitarajiwa kuhudumia ng’ombe 120,280,
mbuzi 136,074 pamoja na kondoo 17,368.
|
|
Mkuu wa wilaya ya Bukoba manispaa Zippora Pangani akikabidhi
Mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Muleba Lamblis Kipuyo katika uwanja wa
Kagondo wilayani Muleba Mei 03,2014.
|
|
Bi.Rechel Steven Kasanda ,mkimbiza Mwenge
wa Uhuru 2014,kitaifa akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Muleba ,Bw.Lambris
Kipuyo katika uwanja wa kagondo Mei 03,2014.
|
Aidha Mkuu wa wilaya ya Bukoba Manispaa
,Bi.Zipporah Pangani amesema mwenge
ukiwa Manispaa ya Bukoba, ulizindua na kukagua miradi
tisa yenye thamani y Sh. Bilioni 2 na Milioni 432, 203,940 katika sekta ya Elimu,Barabara ,Maji ,Afya na
Mazingira .
|
Kiongozi wa
mbio za Mwenge wa Uhuru 2014
,Kitaifa akisoma na kukabidhi hundi ya
Sh.Milioni 1 na Laki 500,000/- kama mchango wa mbio za mwenge katika miradi ya
maendeleo wilayani Muleba.
|
|
Kiongozi wa
mbio za Mwenge wa Uhuru 2014
,Kitaifa akikabidhi hundi ya Sh.Milioni
1 na Laki 500,000/- kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Rutabo , kama mchango wa mbio za mwenge kwa shule hiyo.
|
|
Picha Juu na Chini ni sehemu ya Mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu Rushwa kutoka kwa Wanafunzi wa Klabu ya Kupinga na Kupambana na Rushwa katika Shule ya Sekondari Rutabo ,iliyopo Kata ya Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera , wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 ulipofika na Kufungua Bweni la Wavulana Mei 03,2014 lililojengwa kwa Thamani ya Sh.Milioni 58.5...Picha zote Na:-Shabani Ndyamukama-Muleba.
|
No comments:
Post a Comment