Bayern
Munich manager Pep Guardiola
watches on
as his side are beaten
by Real
Madrid.
|
“Kila kitu kinatokea katika mpira kutokana na kucheza vizuri. Nimefungwa mara nyingi katika kazi yangu na hii ni mojawapo”. Guardiola amewaambia waandishi wa habari.
“Tulifungwa mabao mengi, lakini tulicheza kwa kiwango kikubwa na ndio sababu ya kupoteza”.
“Hakuna sababu nyingine, huu ndio mpira”.
“Unapocheza vibaya, unafungwa mabao mengi. Tuliingia na nguvu, tungeweza kufunga kwa nafasi tulizopata, lakini hatukuweza”.
“ Kucheza kwetu vibaya ndio sababu pekee ya kufungwa”.
Kabla ya mechi hiyo, nyota wa zamani wa soka la Ujerumani, Stefan
Effenberg alionesha wasiwasi wake kama falsafa ya Pep Guardiola itaisaidia
Bayern Munich kutwaa ubingwa wa UEFA, wakati huu ambapo mchezaji muhimu Frank
Ribery yupo katika kiwango cha chini.
Effenberg anaamini falsafa ya sasa ya Bayern ya kupiga pasi nyingi
haikuweza kuwasaidia Bernabeu na alikuwa na wasiwasi katika mechi ya leo.
Kipigo cha mabao 4-0 kimethibitisha mawazo ya gwiji huyo wa soka la Ujerumani.
Bayern imefanikiwa kutwaa kombe la dunia la klabu na Bundesliga msimu huu, na wamebakiwa na kombe la mwisho la DFB-Pokal mei 17 dhidi ya Borussia Dortmund.
Hii itakuwa kama marudio ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka jana.
Tangu mwaka 2002 wakati Zinedine Zidane alipofunga moja ya magoli mazuri
kabisa katika historia ya Champions League na kuiwezesha Real Madrid kutwaa wa
ulaya kwa mara ya mwisho mpaka leo – klabu hiyo ya Hispania imetumia zaidi ya Paundi
830million kwa ajili ya usajili wa wachezaji mbalimbali ili kuweza kutimiza
ndoto yao ya kuwa timu ya kwanza ya ulaya kufikisha idadi ya makombe 10 ya
ulaya.
Ronaldo baada ya akifunga mabao mawili jana usiku huu amevunja rekodi ya Lionel
Messi kwa kufikisha mabao 16 katika msimu mmoja wa UEFA.
Real Madrid wamefuzu kwa mara ya kwanza fainali tangu walipofanya hivyo mwaka 2002 na kutwaa kombe na sasa wanatarajia kukutana na Chelsea au Atletico Madrid ambazo zitapambana leo (April 30,2014) katika uwanja wa Stamford Bridge.
Mechi ya kwanza katika dimba la Vicente Calderon mjini Madrid, Chelsea
walilazimisha suluhu ya bila kufungana, hivyo wanahitaji bao 1-0 ili kufuzu
fainali.
Aidha Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristian Ronaldo ameweka rekodi ya
kufunga mabao 16 katika msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mwingine aliyekuwa na mabao mengi zaidi alikuwa ni Lionel Messi aliyekuwa
amewahi kufunga 14.
UEFA
Champions League leading scorers season by season
2012/13: Cristiano Ronaldo (Real Madrid CF) – 12 goals
2011/12: Lionel Messi (FC Barcelona) – 14
2010/11: Lionel Messi (FC Barcelona) – 12
2009/10: Lionel Messi (FC Barcelona) – 8
2008/09: Lionel Messi (FC Barcelona) – 9
2007/08: Cristiano Ronaldo (Manchester United FC) – 8
2006/07: Kaká (AC Milan) – 10
2005/06: Andriy Shevchenko (AC Milan) – 9
2004/05: Ruud van Nistelrooy (Manchester United FC) – 8
2003/04: Fernando Morientes (AS Monaco FC) – 9
2002/03: Ruud van Nistelrooy (Manchester United FC) – 12
2001/02: Ruud van Nistelrooy (Manchester United FC) – 10
2000/01: Andriy Shevchenko (AC Milan) – 9
1999/00: Mário Jardel (FC Porto), Rivaldo (FC Barcelona), Raúl González (Real Madrid CF) – 10
1998/99: Andriy Shevchenko (FC Dynamo Kyiv), Dwight Yorke (Manchester United FC) – 8
1997/98: Alessandro Del Piero (Juventus) – 10
1996/97: Milinko Pantić (Club Atlético de Madrid) – 5
1995/96: Jari Litmanen (AFC Ajax) – 9
1994/95: George Weah (Paris Saint-Germain) – 7
1993/94: Ronald Koeman (FC Barcelona), Wynton Rufer (SV Werder Bremen) – 8
1992/93: Romário (PSV Eindhoven) – 7
No comments:
Post a Comment