![]() |
|
Jinsi
Terminal III ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere utavyoonekana
baada ya ujenzi wake kukamilika mwaka 2016.
|
![]() |
|
Rais Kikwete
akipata maelezo ya ujenzi wa Awamu ya Tatu ya Uwanja wa Kimataifa wa Julius
Nyerere wa Dar es Salaam kwenye eneo la Uwanja huo.
|
![]() |
|
Mkurugenzi
Mkuu Kampuni ya Kuhudumia ndege, abiria
na mizigo ya Swissport Tanzania Tanzania
Limited, Gaudence Temu (kulia) na wadau wengine.
|
![]() |
|
Wadau wa
Kipawa na vitongoji vyake......'
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameiamuru Wizara
ya Uchukuzi na taasisi zake kuchukua hatua za mara moja kukomesha aibu ya
viwanja vya ndege vya Tanzania kutumika katika uchochoro wa kupitisha na kusafirisha
madawa ya kulevya.
Aidha,Rais
Kikwete amesema ukweli kuwa madawa ya kulevya yanazidi kupita katika viwanja
vya ndege za Julius Nyerere International Airport (JNIA) na ule wa Kilimanjaro
International Airport (KIA) unazidi kuchafua heshima na jina la Tanzania.
Rais
Kikwete alikuwa anazungumza leo, Alhamisi, Aprili 24, 2014, kabla ya kuweka jiwe
la msingi kwenye ujenzi wa Awamu ya Tatu ya Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere
wa Dar es Salaam kwenye eneo la Uwanja huo.
Rais
ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Uwanja huo muda mfupi baada ya kuweka jiwe
la msingi kwenye Ujenzi wa Hospitali ya Kisasa ya Kufundishia na Kutoa Huduma
katika eneo la Mlongazila, eneo la Kibamba, Dar Es Salaam. Shughuli zote mbili
ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano.
“Siridhishwi
na hali ya usalama katika viwanja hivi viwili na matukio ya kusikia madawa yametokea
Tanzania kupitia viwanja vyake na yamekamatwa huko Australia yanachafua sana
jina la nchi yetu.
Badala ya kuchukua hatua kukomesha jambo hili tunakwenda
mbele, tunakwenda nyuma…mbele, nyuma.
Hili
haliwezi kuruhusiwa kuendelea. Ni jambo la kutia simanzi sana,”amesema Rais
Kikwete na kuendelea:-“Mmeyasema wenyewe…leo kiwanja hiki kinapitisha abiria
milioni 2.5 kwa mwaka, mkifikisha abiria milioni sita si mtakuwa soko huria
kabisa…..mara leo mwanamuziki huyu kakamatwa Afrika Kusini…mara kesho
yule….limalizeni hili haraka.
Nataka
tuongeze usalama sana katika viwanja hivi viwili…. vimekuwa kama uchochoro.”
Rais
Kikwete amemtaka Waziri wa Uchukuzi
kumjulisha ni maofisa gani wa Idara za Serikali wanahusika kupitisha
madawa hayo kwenye viwanja hivyo:
“Kama
kuna maofisa wa ushuru, ama maofisa wa uhamiaji, ama maofisa wa polisi ama maofisa
wa uwanja wa ndege ambao wanashiriki katika mchezo huu wa kupitisha madawa haya
nipeni orodha yao, nitawaondoa kazini. Tusifanye masihara na hili,
linatuaibisha sote.
Tusiwaonee
aibu watu katika jambo hili.”
Imetolewa
na:-Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
24 Aprili, 2014






.jpg)
.jpg)








No comments:
Post a Comment