MVUA:Tazama Picha Hali inavyokuwa tete katika barabara hii…Nyakanazi-Kibondo-Kasulu..Mvua ikinyesha..’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 01, 2014

MVUA:Tazama Picha Hali inavyokuwa tete katika barabara hii…Nyakanazi-Kibondo-Kasulu..Mvua ikinyesha..’


Muonekano wa Matope na kukwama kwa Basi la Abiria katika Barabara ya Nyakanazi -Kigoma kupitia wilaya za Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, huwa kero kubwa hasa msimu wa Mvua kwa kusababisha magari kuteleza na mengine kukwama kwa sababu ya Matoke kama Picha zinavyoonesha....na bila shaka kunahaja ya kuitazama na kuipa kipaumbele barabara hiyo ili kuondoa kero za kiusafirishaji.


Labda pengine kukamilika kwa ujenzi wa daraja katika Mto Malagarasi, mkoani Kigoma huenda ukasaidia Magari kupita huko yakipita kutoka kati ya Manyoni – Itingi – Tabora hadi Kigoma kupitia katika Daraja hilo la Kikwete, hali ambayo awali ililazimu kupitia barabara ya Manyoni – Singida – Nzega – Kahama – Nyakanazi – Kibondo – Kasulu hadi Kigoma.


Aidha wakati wa sherehe za miaka 36 ya CCM- zilizofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma….Akizungumzia kero ya muda mrefu ya Barabara ya Nyakanazi- Kigoma kupitia wilaya za Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi - CCM, Bw.Abdulrahman Kinana alisema, barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami kama ilivyoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni.

"Wananchi ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami lazima utafanyika kwa sababu ahadi hii ipo katika ilani ya CCM na ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete hivyo msiwe na shaka na hili, nitamkumbusha Rais wetu, Jakaya Kikwete na bila shaka atalipa mkipaumbele swala hili", alisema Kinana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad