![]() |
|
Kabla
hajaanza, wajumbe walianza kuzomea wengine wakipiga kelele ndipo Mwenyekiti wa
Kudumu wa Bunge hilo,Bw. Samuel Sitta alipoamua kusitisha shughuli za Bunge
mpaka itakapotangazwa.
|
BARUA
YA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) KWA
MWENYEKITI
WA BUNGE MAALUM, MHESHIMIWA SAMWEL J. SITTA,
KUHUSU
UKIUKWAJI WA KANUNI ZA BUNGE MAALUM
Mheshimiwa
Mwenyekiti,
Sisi
ambao majina yetu yameorodheshwa hapa chini ni Wajumbe
wa
Bunge Maalum ambao tunatokana na vyama vya CHADEMA,
CUF,
NCCR Mageuzi, DP, UDP, CHAUSTA, CHAUMA, NRA, NLD na
CCK
pamoja na Wajumbe walioteuliwa kutokana na makundi
yaliyotajwa
katika kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria ya Mabadiliko
ya
Katiba, Sura ya 83.
Tumeunda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(‘UKAWA’)
wenye lengo la kuhakikisha kwamba mchakato wa
sasa
wa Katiba katika Mkutano huu wa Bunge Maalum
unapelekea
nchi yetu kupata Katiba Mpya na bora kwa ajili ya
nchi
yetu.
Kwa
sababu ya mwendelezo wa matukio ya ukiukwaji wa
makusudi
wa Kanuni za Bunge Maalum, 2014, ambao umefanyika
tangu
ulipoapishwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, kama
tunavyoonyesha
hapa, tunapenda kukufahamisha kwamba
hatuko
tayari kuendelea kukaa kimya wakati unaendelea kuvunja
Kanuni
za Bunge Maalum na kupelekea Mkutano wa Bunge
Maalum
kuwa hatarini kuvunjika.
Katika kipindi cha siku nne tangu
umeapishwa
kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum umefanya
maamuzi
yafuatayo yanayodhihirisha ukiukwaji wa Kanuni:-
1.
Tarehe 14 Machi, 2014, mara tu baada ya kuapishwa
ulitangaza
kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba
atawasilisha Rasimu ya Katiba siku ya Jumatatu,
yaani
leo.
Aidha, ulitangaza kwamba baada ya Mwenyekiti
wa
Tume kuwasilisha Rasimu, kutakuwa na kipindi cha siku
tatu
kwa Wajumbe wa Bunge Maalum kufanya mjadala wa
jumla
juu ya Rasimu kwa lengo la ‘kufungua vifua vyao.’ Vile
vile,
ulilitaarifu Bunge Maalum kwamba baada ya hapo
Mheshimiwa
Rais atakuja kulihutubia Bunge Maalum kati ya
siku
ya Jumanne au Jumatano.
2.
Licha ya Wajumbe kadhaa wa Bunge Maalum kukuomba
ubadilishe
msimamo wako juu ya masuala haya, tarehe 15
Machi
uliendeleza msimamo huo na ukaongeza kwamba
Mwenyekiti
wa Tume atawasilisha Rasimu ya Katiba kwa
muda
usiozidi dakika sitini na baada ya hapo kutakuwa na
siku
tatu za semina itakayoongozwa na wataalamu kutoka
nje
ya nchi yetu na baadaye ndiyo Mgeni Rasmi atakuja
kulihutubia
Bunge Maalum.
3.
Leo tarehe 17 Machi baada ya malalamiko ya Wajumbe
kadhaa
umesema kwamba umeshauriana na Mwenyekiti
wa
Tume jana tarehe 16 Machi na mmekubaliana kwamba
muda
wa saa mbili (dakika mia moja ishirini) zitamtosha
Mwenyekiti
wa Tume kuwasilisha Rasimu ya Katiba.
Hii
inathibitisha
kwamba ulipopanga muda wa dakika sitini kwa
ajili
hiyo siku ya tarehe 15 Machi ulikuwa hujashauriana na
Mwenyekiti
wa Tume kama inavyotakiwa na Kanuni za
Bunge
Maalum. Aidha, kwa taarifa tulizo nazo, inaelekea
Mwenyekiti
wa Tume analazimishwa kukubaliana na muda
ambao
wewe mwenyewe na nguvu nyingine zilizo ndani na
nje
ya Bunge Maalum mmempangia.
Kwa
maoni yetu, yote haya ni ukiukwaji wa makusudi wa
Kanuni:-
(a)
Kanuni ya 7(1)(g) na (h) ya Kanuni za Bunge Maalum
imeweka
mpangilio wa shughuli zote za Bunge Maalum
ambapo
‘hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi’, i.e., Rais
wa
Jamhuri ya Muungano au Rais wa Zanzibar,
itafuatiwa
na ‘uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba.’ Kwa
jinsi
ya mpangilio wa shughuli uliowekwa na Kanuni ya
7(1),
uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba kabla ya hotuba
ya
ufunguzi ya Mgeni Rasmi ni ukiukwaji wa Kanuni za
Bunge
Maalum na, kwa vyovyote vile, kunatoa picha
kwamba
Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuja
Bungeni
kama mchangiaji wa hoja badala ya kuja
kama
Mkuu wa Nchi kwa lengo la kufungua Bunge
Maalum;
(b)
Kanuni ya 47(a) inaelekeza kwamba “Mwenyekiti
baada
ya kushauriana na Mwenyekiti wa Tume
watapanga
muda unaofaa kwa ajili ya Mwenyekiti wa
Tume
kuwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge
Maalum.”
Pamoja na kwamba kanuni hiyo imeanza
kwa
maneno ‘isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo
kwenye
Kanuni hizi au Mwenyekiti ameelekeza
vinginevyo’,
ufahamu wetu wa Kanuni za Bunge
Maalum
unatuelekeza kwamba Mwenyekiti wa Bunge
Maalum
hana uwezo kikanuni wa kujipangia yeye
mwenyewe
muda ambao Mwenyekiti wa Tume
atahitaji
kwa ajili ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba.
Muda
huo unatakiwa kupangwa kwa pamoja baada
ya
mashauriano baina yao.
(c)
Kwa mujibu wa kanuni ya 31(3), “baada ya Rasimu
kuwasilishwa
… Mwenyekiti atatangaza majina ya
wajumbe
wa kila Kamati … na kila Kamati itatekeleza
majukumu
yake kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa
na
Kanuni hizi.” Aidha, kwa mujibu wa mpangilio wa
kanuni
ya 32, baada ya Kamati kuundwa, Rasimu
itajadiliwa
katika Kamati na baadaye katika Bunge
Maalum.
Kwa mtiririko wa Kanuni ulivyo, hakuna namna
yoyote
halali kwa Bunge Maalum kufanya semina ya
wataalamu
wa ndani au nje ya nchi kwa lengo la
wajumbe
kufungua vifua vyao au kwa lengo lingine
lolote.
(d)
Matumizi mabaya ya kanuni ya 85 inayohusu mamlaka
ya
kutengua kanuni. Ijapokuwa kanuni ya 85(1)
inatamka
kwamba “… kanuni yoyote inaweza
kutenguliwa
kwa madhumuni mahsusi …”, kanuni hiyo
imefungwa
na masharti ya kanuni ya 85(4) inayoelezea
mazingira
yanayoweza kusababisha kanuni itenguliwe.
Kwa
kifupi, kanuni inaweza kutenguliwa kwa ajili ya
kuahirisha
kikao au kuongeza muda wa shughuli au
kuongeza
orodha ya shughuli yoyote ambayo
haikuwepo
kwenye mpangilio wa shughuli za siku hiyo.
Nje
ya mazingira hayo, Bunge Maalum haliwezi
kutengua
kanuni zake.
Kwa
sababu ya ukiukwaji huu wa Kanuni za Bunge Maalum
tunapenda
kukujulisha kwamba sisi wanachama wa UKAWA
hatuko
tayari kuunga mkono, na tutapinga kwa kadri ya
uwezo
wetu mambo yafuatayo kufanyika ndani ya Ukumbi
wa
Bunge Maalum:-
(i)
Uwasilishaji wa Rasimu ya Katiba na Mwenyekiti wa
Tume
kabla ya hotuba ya ufunguzi wa Bunge
Maalum
na Rais wa Jamhuri ya Muungano au Rais
wa
Zanzibar;
(ii)
Semina yoyote itakayoongozwa na wataalamu wa
ndani
au nje ya nchi yetu kama ulivyolitangazia
Bunge
Maalum;
(iii)
Hotuba ya Mgeni Rasmi endapo itafuatia uwasilishaji
wa
Rasimu ya Katiba;
(iv)
Jambo lingine lolote linalokiuka Kanuni za Bunge
Maalum.
Tunatarajia
kwamba utayapa masuala haya tafakuri ya kutosha ili
uweze
kufanya maamuzi kwa kutumia Kanuni za Bunge Maalum.
Tunaamini
utatumia busara na hekima ili kuliepusha Taifa letu na
fedheha
ya vurugu zisizokuwa na sababu ndani ya Bunge
Maalum.
Tunatanguliza
shukrani zetu za dhati.
Chanzo
JF.







No comments:
Post a Comment