|
Mtoto Halidi Mustapha Mohamed (10) akiwa amejeruhiwa baada ya kumwagiwa
tindikali yeye pamoja na baba yake.
|
Sheikh wa Msikiti Mkuu wa Bondeni mkoani Arusha,Mustapha Mohamed Kiago na
mwanaye Khalid Mustapha mwenye umri wa miaka 10, wamemwagiwa kimiminika
kinachodhaniwa kuwa ni tindikali wakati wakiingia msikitini jana Februari 28,2014.
Sheikh Kiago amejeruhiwa shingoni
na mtoto wake ameumizwa machoni na wote wanatibiwa katika hospitali ya mkoa wa
Arusha ya Mount Meru.
Sheikh Kiago amesema amemwagiwa tindikali hiyo jana majira ya saa 11.10
alfajiri wakati anashuka ngazi kuingia msikitini kuongoza sala ya alfajir.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Bw Japhet Lusingu,
akizungumzia tukio hilo, amesema polisi ina taarifa za tukio hilo na kwamba
inaendelea na uchunguzi.






No comments:
Post a Comment