|
Mgombea Ubunge Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini,
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw.Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa na
wafuasi wa chama hicho jana March 16,2014, usiku katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa baada
kutangazwa matokeo ya awali yasiyo rasmi .Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka
na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata zote 13 zilizoko kwenye jimbo hilo la
Kalenga.
|
Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Kalenga - Iringa vijijini yametangazwa
rasmi jana March 16,2014, usiku na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Iringa,kuwa chama cha Mapinduzi ( CCM)
kilipata jumla ya kura 22945,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA),Kilipada idadi ya jumla kura 5800 na chama cha CHAUSTA kilipata kura
143.
Hivyo chama cha CCM kilishinda kwa asilia 79.4,CHADEMA asilimia 20.1 na
CHAUSTA asilimia 0.5.Matokeo hayo ni ya jumla kwa Kata 13 za jimbo hilo.
|
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, Watu 71, 765
walitarajiwa kupiga kura katika vituo 216, lakini kwa Mujibu wa Waandishi wa Habari waliokuwa
wakifuatilia uchaguzi huo mdogo wa Ubunge, walisema kulikuwa na idadi ndogo ya
watu waliojitokeza katika baadhi ya vituo, huku wengi wakilalamika kushindwa
kupiga kura kutokana na kupoteza vitambulisho vyao.
|
No comments:
Post a Comment