Wanawake wa kiislamu wametakiwa kutambua
umuhimu wao katika dini ikiwa ni pamoja na kulinda maadili kwa kuzingatia
mafundisho ya Mwenyezi Mungu na mtume Mohamadi SAW.
Wito huo umetolewa
Februari 14,2014, na Kiongozi wa Waislamu wilayani Ngara mkoani Kagera ,Shekhe
Rajabu Abdallah Msabaha wakati akifungua kongamano la wanawake wa kiislamu lililokuwa likifanyika kwa siku tatu katika mtaa wa Benaco ulioko
wilayani Ngara.
Kiongozi wa Waislamu
wilayani
Ngara mkoani
Kagera ,
Shekhe
Rajabu Abdallah Msabaha.
|
Shekhe Msabaha alisema kuwa wanawake wanao wajibu wa kujifunza dini yao
kwa kuhakikisha wanafuata na kuzingatia maadili mema ili kuweza kurithisha
vizazi vinavyotoka katika migongo na matumbo yao.
Alisema
malezi na maadili mema katika familia yanategemea wanawake ,kwani ndio walimu
wa kwanza kuwafunza watoto katika kufuata misingi inayokubalika katika jamii
waliyomo na dini yao.
“Kwa
asilimia kubwa akina mama ni walezi wa
watoto tunao wazaa hivyo mkipata elimu ya dini kwa hakika
mtaisambaza kwa familia na watoto kuwa
na maadili ya kiislamu kisha kupatikana
nusura kutoka kwa Allah S.W”. Alisema Sheikh Rajabu.
Kwa upande
wake Imamu wa msitiki wa Istikhama kutoka Ngara mjini ,Ustadhi,Athumani
Abubakari Ally aliwahimiza wanawake hao
kufanya ibada za dini yao bila kujivunia, ibada zinazofanywa na wanaume ama watoto walioko katika familia.
Alisema
kuwa wanawake wanatakiwa kupata elimu ya
kufanya ibada katika taratibu na misingi ya dini hasa kujua namna ya
kusali sala mbalimbali na masharti yake ili kuepuka kufuata matendo bila
elimu inayotakiwa.
“Mafundisho
ya Q’urani ambayo ni kitabu cha Allah na hadithi za Mtume SAW ni kuhakikisha
wanawake na wanaume wanakuwa na maadili kwa misingi ya imani ya dini
pamoja na kuvaa mavazi ya kusitiri miili kiislamu”.Alisema Athuman Ally.
Aidha
mwenyekiti wa Wanawake wa Kiislamu
wilayani Ngara, Bi Zaria Mohamudu alisema malengo ya kongamano hilo ni kuwafunza wanawake kuzijua
haki zao kidini ,kijamii na kuondoa vitendo vya unyanyasaji
kwenye familia.
Alisema kuwa
jambo lingine ni kuhakikisha wanapata elimu ya ujasiliamali na kujikwamua kiuchumi
kwa kutumia misingi inayokubaliwa na dini
ya kiislamu kwa kuepuka kutoa na
kuchukua mikopo yenye riba.
Kongamano
hilo lilihudhuriwa na wahadhiri wa kiislamu kutoka wilayani Ngara na wilaya
nyingine mkoani Kagera pamoja na
waliotokea Mwanza na Nairobi kwa kutoa mada za ndoa taraka na mirathi
kwa wanawake na haki zao katika familia.
Habari /Picha NGARA:
Na:- Shaaban Nassibu Ndyamukama.
No comments:
Post a Comment