Jumapili Februari 16,2014, huko
Beira, Nchini Msumbiji, Azam FC ya Tanzania ikicheza Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Awali ya
Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho, ilifungwa Bao 2-0 na Ferroviario de
Beira na kutupwa nje kwa Jumla ya Bao 2-1.
Wiki iliyopita
huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC
iliifunga Ferroviario de Beira Bao 1-0.
Hapo Jana Jumamosi Februari 15,2014,
Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Michuano hii ya Kombe la Shirikisho, Chuoni,
walifungwa 2-1 Mjini Zanzibar na How Mine ya Zimbabwe na kutolewa kwa Jumla ya
Bao 6-1 kwani Wiki iliyopita huko Zimbabwe walinyukwa Bao 4-0.
Timu nyingine ya
Zanzibar inayocheza Michuano ya Afrika, kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI, ni KMKM ya
Zanzibar ambao katika mchezo huo timu ya KMKM imeshinda bao 2--0. na kutolewa
katika michuano hiyo kwa kufungwa mchezo wa ugenini kwa mabao 3--0,ilihitaji
ushindi wa mabao 4 kwa bilo indi isonge mbele katika michuano hiyo ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan.
Timu pekee ya
Tanzania ambayo imefanikiwa kusonga kutoka Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ
LIGI ni Yanga SC ambayo Jana Jumamosi Februari 15,2014,huko Comoro waliibonda Komorozine de Domoni Bao 5-2
na kuitupa nje kwa Jumla ya Bao 12-2 kwani waliifunga 7-0 Wiki iliyopita Jijini
Dar es Salaam.
Yanga SC sasa
watacheza Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Al Ahly ya Misri
ambao ndio Mabingwa Watetezi na Mechi hizi zitachezwa kati ya Februari 28 na
Machi 2 na Marudiano ni kati ya Machi 7 na 9 Mwaka huu.
Kwenye Raundi ya
Kwanza ya Kombe la Shirikisho, Ferroviario de Beira watakutana na ZESCO ya
Zambia.
No comments:
Post a Comment