Kala ameongea na tovuti ya Times Fm na kuelezea jinsi ambavyo tukio hilo lilivyomsikitisha, na kudai kuwa ingawa hakuwasiliana na wasanii hao anaamini kabisa kuwa kupitia maelezo anayoyatoa kwenye media wameelewa kuwa sio yeye bali ni watu walioiteka akaunti yake ya Facebook.
“Jana limezuka lingine la kupost mikopo sijui nini halafu wakawataja na wasanii na hiyo ndio mbaya zaidi kwa sababu wanawagombanisha wale wasanii, halafu wanawagombanisha wale wasanii kupitia mimi.
Kwa hiyo kwa mtu mwingine ambaye hana uelewa zaidi, au ukikuta msanii mwenyewe akawa hana uelewa zaidi unaweza kujikuta na yeye anakumaindi, yaani kwa ujumla sio kitu kizuri.” Kala Jeremiah ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Lakini hayo yote mimi namuachia Mungu kwa sababu Mungu ndiye anayenijua mimi kiundani. Hawa watu ni binadamu wanafanya hayo lakini ipo siku…kwa sababu wote tuko chini ya jua, hawawezi kujua mimi nilihustle kiasi gani kuifikisha hiyo page hapo halafu mtu anaitumia kufanya anavyotaka yeye, anaitumia anavyotaka yeye, anaandika vitu anavyotaka yeye.” Ameongeza.
Amewataka watanzania kufahamu kuwa ile page ya Facebook yenye ‘likes’ zaidi ya 50,000 kwa sasa sio yake tena na kwamba kuna wahuni ambao wanaitumia.
Katika ukurasa huo wa facebook aliopokonywa Kala mwaka jana, wezi hao wameanza kuwatapeli watu kwa kuonesha kuwa Kala Jeremiah anatangaza kutoa mikopo kwa riba nafuu.
Katika hatua nyingine, rapper huyo yuko katika hatua za mwisho za kushuti video ya Remix ya wimbo wake Wale Wale, aliyofanya na Juma Nature, Young Killer na Ney Lee.
Usikose kusikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm kwa undani wa habari hii, na utamsikia Kala Jeremia akifafanua kwa undani jinsi alivyopata hasara kufuatia kuibiwa kwa ukurasa wake wa Facebook.
Sorce:-Times.
No comments:
Post a Comment