Baada ya kupotea tangu Desemba mwaka jana yale Mashindano makubwa kwa Vilabu
Barani Ulaya, UEFA CHAMPIONZ LIGI 2013/2014, yanarudi tena kuanzia Jumanne Februari
18 kwa Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Bigi Mechi Siku hiyo
ni kati ya Manchester City na Barcelona.
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumanne Februari 18 ,2014.
22:45 Manchester City v FC Barcelona
22:45 Bayer 04 Leverkusen v Paris
Saint-Germain
Jumatano Februari 19,2014.
22:45 AC Milan v Atletico de Madrid
22:45 Arsenal FC v Bayern Munich
MANCHESTER CITY FC V FC BARCELONA
-Timu hizi hazijakutana katika
Mashindano rasmi lakini zimeshacheza Mechi za Kirafiki mara 6.
-Barca walishinda Mechi 3 za kwanza,
wakafungwa ya nne kwa Penati baada ya Sare ya 1-1 na Man City kushinda Mechi
mbili za mwisho ikiwemo ile ya Tarehe 10 Agosti 2003 , Siku ya Ufunguzi wa City
of Manchester Stadium, na City kushinda Bao 2-1 kwa Bao za Nicolas Anelka na
Trevor Sinclair na la Barca kufungwa na Javier Saviola.
Kwenye Kikosi cha Barca Siku hiyo walicheza
Carles Puyol na Xavi Hernández na Iniesta kuingia Kipindi cha Pili.
Mechi ya mwisho kukutana ni ile ya
Kirafiki Agosti 2009 ambayo Man City walishinda 1-0 kwa Bao la Martin Petrov na
Siku hiyo Yaya Touré, ambae sasa yuko City, alichezea Barca na Mchezaji pekee
wa City hivi sasa aliecheza Siku hiyo ni Pablo Zabaleta.
BAYER 04 LEVERKUSEN V PARIS
SAINT-GERMAIN
-PSG walifunga Bao 16 kwenye hatua
ya Makundi lakini Leverkusen hawajawahi kufungwa na Klabu yeyote toka France
katika Mechi mbili za Mtoano kwenye Mashindano ya Ulaya.
ARSENAL FC V FC BAYERN MÃœNCHEN
-Msimu uliopita, Bayern waliichapa
3-1 Arsenal Nyumbani kwao Emirates katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano
ya Timu 16 ya Mashindano haya.
-Hii na mara ya 4 kwa Bayern kucheza
England katka Miezi 12 iliyopita na wameshinda Mechi 3 ikiwemo Fainali ya UCL
walipowafunga wenzao Borussia Dortmund Mwezi Mei Mwaka Jana Uwanjani Wembley.
AC MILAN V CLUB ATLÉTICO DE MADRID
-Kocha mpya wa AC Milan, Clarence
Seedorf ameshatwaa Kombe la UCL akiwa na AFC Ajax, Mwaka 1995, Real Madrid
CF,1998, na akiwa na AC Milan, Miaka ya 2003 na 2007 akiwa ndie Mchezaji pekee
kutwaa Kombe hili akiwa na zaidi ya Klabu mbili tofauti.
FC ZENIT V BORUSSIA DORTMUND
-Zenit wapo hatua hii kwa mara ya
pili katika Historia yao lakini wamefika hapa wakati wameambua Pointi 6 tu
hatua ya Makundi na hizo ni Pointi chache katika Historia ya UCL kufuzu kuingia
Hatua ya Mtoano.
Kwenye Hatua ya Makundi walitoka
Sare Mechi zao zote 3 za Nyumbani kwa kutoka 0-0 na FK Austria Wien na 1-1 na
FC Porto na Atlético Madrid.
OLYMPIACOS FC V MANCHESTER UNITED FC
-Man United wameshinda Mechi zote 4
walizokutana na Olympiacos huko nyuma kwa kushinda 2-0 Ugenini na 3-0 Old
Trafford Hatua ya Makundi ya UCL Msimu wa 2001/02 na kushinda 4-0 Old Trafford
na 3-2 huko Piraeus Msimu uliofuatia wa UCL.
Ryan Giggs, ambae alicheza Mechi
zote hizo 4, alifunga katika Mechi zote zilizochezwa Old Trafford.
FC SCHALKE 04 V REAL MADRID CF
-Real Madrid wameshinda mara moja tu
katika Mechi 25 huko Nchini Germany, wakifungwa mara 18 ikiwemo kipigo cha 4-1
Msimu uliopita walipotwangwa na Borussia Dortmund kwenye Mechi ya Kwanza ya
Nusu Fainali.
Mechi pekee Real waliyoshinda huko
Germany ni Bao 3-2 walipocheza na Bayer Leverkusen Msimu wa 2000/01.
GALATASARAY AÅž V CHELSEA FC
-Straika wa Galatasaray, Didier
Drogba, aikuwa Chelsea kati ya 2004 na 2012 – akicheza chini ya José Mourinho
kuanzia Juni 2004 mpaka Septemba 2007 – na kufunga Bao 100 katika Mechi
226 za Ligi na kutwaa Ubingwa wa Ligi mara 3, FA CUP 4, Kombe la Ligi mara 2 na
Mechi yake ya mwisho kwa Chelsea ni Fainali ya UCL Mwaka 2012 dhidi ya Bayern
Munich ambapo kwenye Mikwaju Mitano ya Penati, Penati yake ya mwisho ndio
iliwapa Chelsea Ubingwa wa Ulaya.
UEFA CHAMPIONZ LIGI 2013/2014.
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumanne Februari 25 ,2014.
20:00 Zenit St. Petersburg v BV
Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester
United
Jumatano Februari 26 ,2014.
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v
Chelsea FC
No comments:
Post a Comment