“Kwa dimbwi
hili lililojaa maji , magonjwa ya kipindupindu ,minyoo na fungasi yako nje nje
na kuhatarisha afya za watoto wetu hasa wale wa miaka 5 hadi 15 kwa kutumia maji hayo kuyachezea ‘’.
|
Baadhi ya
wakazi wa mji huo wa Benaco wanasema maji hayo yamekuwepo takribani miezi
miwili kutokana na sehemu yalikokuwa yakipita kuzibwa baada ya kumwaga kifusi cha changarawe.
|
Diwani wa
kata ya Kasulo Dr. Philbert Kiiza
alipoulizwa juu ya dimbwi hilo, alisema mamlaka ya kuondoa maji hayo ni
Tanroads makao makuu ya mkoa wa Kagera
kwa kshirikiana na idara ya ujenzi na ardhi wilayani Ngara.
Alisema kuwa
idara ya ardhi ilisha weka mipango miji kwa kugawa viwanja na wenye navyo kuwa
na hati miliki hivyo baadhi ya meneo hayako kwenye mamlaka ya kijiji ama kata.
“Jirani wa
msikiti aliyemwaga kifusi eneo la msikiti lisichukuliwe kuwa vita baina ya
waislamu na wakristu kwa kuwa yeye si
mwislamu bali ni kukaa na kutatua kero hiyo kwa njia ya amani”.Alisema Afisa
mtendaji.
Hata hivyo
aliahidi kufuatilia kwa meneja wa Tanroads mkoani Kagera kwani maji hayo hayasumbui waumini wa msikiti huo
bali wananchi wote ambao nao wana hofu ya maji hayo kudhuru maisha ya kila mmoja wao.
No comments:
Post a Comment