Tazama Taswira ya Semina ya siku Tano ya kuwajengea Uwezo Waandishi wa habari wa Radio Kwizera FM ya wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 20, 2014

Tazama Taswira ya Semina ya siku Tano ya kuwajengea Uwezo Waandishi wa habari wa Radio Kwizera FM ya wilayani Ngara mkoani Kagera.

Muonekano wa baadhi ya staff wa Kituo cha Radio Kwizera FM wilayani Ngara mkoani Kagera wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa kituo hicho wakishiriki semina ya siku tano ambapo kwa Mujibu wa Mkurugenzi wa Kituo hicho Fr.Damas Missanga amesema Semina hiyo inawajengea uwezo/Kuwaongezea ujuzi katika kusaidia Jamii Namna gani  inaweza kunufaika na fursa kupitia Jumuia ya Africa ya Mashariki pamoja na Namna ya Uandishi wa Habari za Kiuchunguzi ili kukuza Demokrasia na Utawala bora na Biashara.

Muwezeshaji wa semina hiyo ni Bw.Fili Karashani muandishi mkongwe wa Habari kutoka Dar es Salaam akiendelea na Darasa lake Juu ya  Namna ya Uandishi wa Habari za Kiuchunguzi pamoja na Biashara.

Mwandishi wa Habari James Jovin Radio Kwizera FM -Kibondo,Saimon Dioniz Radio kwizera-Ngara na Ofisa Masoko Sara Mkongwa wakifatilia kinachofundishwa katika Semina hiyo ya siku tano kwa  baadhi ya staff wa Kituo cha Radio Kwizera FM wilayani Ngara mkoani Kagera.

CEO/Director wa Mwanawamakonda Blog mwenye shati la orange nae ni moja wa washiriki wa semina hiyo akiwa katika majadiliano ya kikundi kilichopewa na jina la Radio Bombastic pembeni yake ni Sara Mkongwa na Ailine Terufukwa.



Joyce Ngallawa amabeye ni mkuu wa uzalishaji Vipindi(Production Officer) akiendelea majadiliano ya kikundi chao kilichopewa jina la Freedonia Broadicasting Coorporation kulia kwake ni Maria Philibert,Amina Semagogwa,Shabani Ndyamukama.


Kikindi cha Majanga FM kikiendelea na majadiliano juu ya uandishi wa habari wakionekana hapo Wiliam Mapanju,Beatha Kisaka,Dotto Bahemu,Godwin Buchard,Erasmus Luziro na Saimon Dionizi.

1 comment:

  1. Poa sana RK team, mbona simwoni Juventus Juvenary? Kila la kheri 2014.
    Naitwa Bigie Anko,
    mdau wa Rulenge

    ReplyDelete

Post Bottom Ad