Taswira ya Ajali ya Lori na NOAH ikiua Watu 13 mkoani Singida. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 20, 2014

Taswira ya Ajali ya Lori na NOAH ikiua Watu 13 mkoani Singida.

Ajali mbaya imetokea leo (Januari 20,2014) huko mkoani  Singida na watu 13 wamefariki dunia baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Isuna mkoani humo.

Habari zinasema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noah na lori ambayo namba zake za usajili hazikupatikana mara moja. 

Watu 13 waliofariki walikuwa katika Noah iliyokuwa ikitokea Itigi na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida. 

Baada ya ajali hiyo, dereva wa lori na msaidizi wake walitokomea kusikojulikana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad