Abiria 48 wanusurika kufa baada ya basi la Shabiby kuanguka mkoani Singida. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 14, 2014

Abiria 48 wanusurika kufa baada ya basi la Shabiby kuanguka mkoani Singida.

Abiria arobaini na nane waliokuwa wakisafiri na basi la shabiby kutoka Mkoani Arusha kuelekea  Mkoani Dodoma wamenusurika kufa huku 28 wakijeruhiwa baada ya basi lao kutaka kulipita lori la mafuta wakati basi lingine la Princes Munaa nalo likiwa linalipita basi la Shabiby  katika mlima Kisaki na kusababisha basi la Shabiby kuanguka.

Wakieleza kondakta wa basi hilo aina ya Yunton lenye usajili wa namba T 930 BUW ambaye amevunjika miguu yote miwili  bwana Thadei Muhando na mkaguzi wa basi la Shabubu bwana Williamu Ofyenge wamesema wakati basi lao lilikuwa liki lipita lori la mafuta gafla waliona basi lingine  liki wapita na kuwa magari matatu katika njia moja  na hatimaye dereva wao alishindwa kulimudu basi lao na kusababisha kupinduka.
Kwa upande wake dereva wa roli la mafuta aina ya benzi lenye usajili wa namba raa 496n na tela lake lenye usajili wa namba rl 0255  ambalo lilikuwa likitokea nchi ya Rwanda bwana Hadimana Benjamini amesema alipitwa na mabasi mawili na moja  likamgonga upande wake na hatimaye kuanguka .


Mganga mfawidhi wa  Hospitali ya Mkoa wa Singida Daktali Banuba Deogratius amethibitisha kupokea majeruhi  ishirini na nane ambao wanapatiwa matibabu na mgonjwa moja ambaye alikuwa kondakta wa basi amevunjika miguu yote miwili na wanampatia matibabu.

Mkuu wa wilaya ya Singida Mwl.Queen Mlozi ambaye alifika katika ajali hiyo pamoja na kuwatembelea majeruhi amewataka madereva wote kuzingatia sheria za barabarani  ilikuweza kunusuru uhai wa watu na majeruhi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad