Soma hukumu ya kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, Bi .Victoire Ingabire kutumikia kifungo cha miaka 15 Gerezani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 14, 2013

Soma hukumu ya kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, Bi .Victoire Ingabire kutumikia kifungo cha miaka 15 Gerezani.

Bi .Victoire Ingabire akiwa mahakamani ambapo Mahakama ya juu zaidi nchini Rwanda imeendeleza hukumu ya kwanza aliyopewa kiongozi huyo wa upinzani nchini humo na kuiongeza kutoka miaka 8 hadi 15 jela.



Mahakama kuu nchini Rwanda imemuhukumu kiongozi wa upinzani nchini humo Bi .Victoire Ingabire kutumikia kifungo cha miaka 15 gerezani baada ya kumkuta na hatia ya uhaini.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya Bi Ingabire kukata rufaa akipinga adhabu iliyotolewa awali ya kutumikia kifungo cha miaka 8 gerezani.

Mahakama imemtia hatiani Bi Ingabire kwa makosa ya ugaidi, kuchochea chuki miongoni mwa raia wa Rwanda na kuhusika na mauaji ya halaiki dhidi ya nchi hiyo mwaka 199.

Awali mwezi Oktoba, Bi Ingabire ambaye ni wa asili ya ki Hutu alipatikana na hatia ya ugaidi, na kukana kutokea mauaji ya kimbari dhidi ya kabila la wa Tutsi.

Mauaji hayo yalifanyika mwaka wa 94 ambapo zaidi ya watu 800 wa kabila la wa Tutsi waliuawa.

Bi Ingabire alikata rufaa dhidi ya hukumu ya awali aliyopewa ya kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na makosa ya uhaini kwa kufadhili makundi ya kigaidi na kuhusika katika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 japo upande wa mashtaka nao ulitaka aongezewe hukumu hiyo na hata kupendekeza apewe hukumu ya maisha gerezani.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeshutumu namna kesi ya Bi Ingabire imeendeshwa.

Bi Ingabire amekumbwa na matatizo na sheria ya Rwanda baada ya kurejea nchini humo mwaka  2009, kutoka Uholanzi alikoishi kwa miaka kadhaa. 

Alieleza wazi nia yake kuwania urais nchini humo lakini hakupata fursa kwani punde tu alipowasili alifunguliwa mashtaka hayo.

Kutokana na kujivuta kwa kesi yake, hakushiriki uchaguzi uliofuata wa mwaka wa 2010. Tangu wakati huo, amekuwa kizuizini. 

Amekuwa akiwakilishwa na wakili kutoka Uingereza ambapo 2010 ambapo ameendelea kusisitiza kuwa hajafanya makosa yaliyoelekezwa kwake na kwamba hukumu hiyo ina msukumo wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad