![]() |
|
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
mjini Dodoma -Alhamis Jioni (Novemba 07,2013).
(picha na Freddy Maro) |
Rais Jakaya Kikwete amesema kwamba Tanzania haina mpango wa kujitoa
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na itaendelea kuwepo kwa
kuzingatia matakwa ya mkataba wa EAC na Itifaki zake,licha ya kutoshirikishwa
kwa baadhi ya mambo.
Aidha Rais Kikwete
amesisitiza kuwa Tanzania ni kati ya zile nchi zinazotaka
ngazi zote za mchakato wa utengamano zitekelezwe moja baada ya nyingine bila
kuruka hata moja na kuongeza kuwa huo sio msimamo wake au Serikali
pekee bali ndio Watanzania walio wengi.
Kauli hiyo ilitolewa Alhamis(Novemba 07,2013) Bungeni mjini Dodoma
wakati Rais Kikwete alipolihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuhusu msimamo wa Tanzania juu ya EAC.
“Napenda kuwahakikishia waheshimiwa wabunge
kuwa hatuna mpango wa kutoka (kama vijana wasemavyo hatoki mtu hapa).
Tupo na tutaendelea kuwepo!,” Napenda kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea
kushiriki katika shughuli za EAC na kuimarisha utengamano wa Afrika Mashariki .
“Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa jumuiya
haidhoofiki wala kufa. Na iwapo itadhoofika au kufa kamwe hatutaki
Tanzania inyooshewe kidole kuwa chanzo wala kichocheo chake.
Ndiyo maana,
hatutachoka kuzungumza na wenzetu kuhakikisha kuwa EAC inaendelea
kustawi,” alisema Rais Kikwete.
Alisema kamati hiyo iliongozwa na Profesa Samwel Wangwe
na katika taarifa yake, ilieleza kuwa asilimia 74.4 ya
Watanzania wanaunga mkono kuwepo kwa Shirikisho lakini ni asilimia 25.4 tu
ndiyo waliunga mkono kuharakishwa kwake.
Rais Kikwete alisema ni lazima ni kutambua
ukweli kuwa kunufaika kiuchumi ndicho kichocheo kikubwa cha nchi kujiunga na
kuendelea kuwa mwanachama wa EAC.
Alisema Tanzania itaendelea kukumbusha umuhimu wa
kufanya mambo yanayojenga na kuepuka yale yanayoweza kubomoa, kama vile
kuheshimu matakwa na masharti ya mkataba ulioanzisha EAC, Itifaki zake na
maamuzi halali ya vikao rasmi na asasi za jumuiya hiyo .
“Tukifanya hivyo Jumuiya ya Afrika ya Mashariki itadumu,
itazidi kustawi na kunufaisha nchi wanachama na watu wake kama yalivyo malengo
na madhumuni ya kuundwa kwake,” alisisitiza.
Rais
Kikwete.
Alisema msimamo na mtazamo
wa nchi , kuundwa kwa Shirikisho iwe ndiyo hatua ya mwisho.
Akizungumzia kuhusu kumekuwepo na madai
Tanzania inachelewesha maendeleo ya jumuiya
hiyo alisema hayana ukweli wo wote.
Huku akiongeza Tanzania haina tatizo na kuharakisha
mchakato wa utengamano, lakini inapata taabu kuruka baadhi ya hatua kabla
hazijakamilika.
Hivyo alizitaka nchi uanachama kuwa
makini katika kila hatua tunayochukua.
Alisema kwa msimamo na mtazamo wa
nchi , suala la Shirikisho liwe ndiyo hatua ya mwisho.
Hata hivyo Rais Kikwete alisema pengine
msimamo wetu kuhusu kuharakisha Shirikisho na masuala ya ardhi, ajira,
uhamiaji,ndiyo yanayotuletea vikwazo.
Hivi
karibu viongozi wa nchi tatu wanachama wa EAC yaani Uganda, Rwanda
na Kenya walikutana bila ya ushiriki wa viongozi wa Tanzania na Burundi.
Viongozi wenzangu hao wamefanya mikutano mitatu yaani Juni 24-25 , 2013
mjini Entebbe, Uganda; Agosti 28, 2013 mjini Mombasa, Kenya na Oktoba 28
, 2013 mjini Kigali, Rwanda.







No comments:
Post a Comment