Hivi ndivyo mwili wa Askofu Moses Kulola ulivyoagwa katika viwanja vya kanisa la EAGT Jijini Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 02, 2013

Hivi ndivyo mwili wa Askofu Moses Kulola ulivyoagwa katika viwanja vya kanisa la EAGT Jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa Pikipiki iliyoongoza msafara ikiwasili viwanja vya kanisa la EAGT, Temeke. 
Marehemu Kulola aliyefariki dunia saa 5:35 (Agost 29,2013) baada ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo na mapafu, alianza kusumbuliwa na maradhi hayo karibu mwaka mmoja uliopita.

Gari lililobeba mwili wa( marehemu )Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God (EAGT), Moses Kulola  aliyefariki dunia katika Hospitali ya African Medical Investment (Ami) iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Maaskofu na wachungaji wakiwa wamejipanga kuupokea mwili huo wakati ukiwasili viwanja vya kanisa la EAGT, Temeke.

Mke wa marehemu, Elizabeth Kulola (wa kwanza kulia) na ndugu wengine (kushoto) wakilia kwa uchungu.

Wajukuu wa marehemu wakiwa na nyuso za huzuni. Katikati ni mwimbaji wa Injili ambaye ni mjukuu wa Kulola, Flora Mbasha akilia.

Watu waliohudhuria viwanjani hapo wakilia baada ya mwili kuwasili.

Jeneza la mwili wa marehemu Moses Kulola likiwa mbele ya waombolezaji. Alikuwa ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God (EAGT),na amefariki  katika Hospitali ya African Medical Investment (Ami) iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar.

Mtumishi wa Mungu, mchungaji Katunzi akitoa neno fupi na kuombea sadaka.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senso,  akisaini  kitabu cha maombolezo.

Mchungaji, Anthony Lusekelo akisaini kitabu cha maombolezo.

Mama Getruda Lwakatare  akisaini kitabu cha maombolezo.

Makamu wa Rais, Gharib Bilal (wa pili kulia), akiingia katika viwanja vya kanisa la EAGT, Temeke jana(Septemba 01,2013) wakati mwili wa mwasisi wa makanisa ya kiroho na mhubiri wa kimataifa,  Dk. Moses Kulola, ulipokuwa ukiagwa kwa ajili ya kusafirishwa kwa mazishi yatakayofanyika mkoani Mwanza wiki ijayo.

  …Akisaini kitabu cha maombolezo.

Askofu wa makanisa ya Pentekoste nchini, David Mwasota, akitoa neno la salamu na jinsi alivyokuwa akimfahamu marehemu Kulola.

Mchungaji Josephat Gwajima akitoa salamu za rambirambi.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God (EAGT), Moses Kulola amefariki dunia  katika Hospitali ya African Medical Investment (Ami) iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Marehemu Kulola aliyefariki dunia saa 5:35 (Agost 29,2013) baada ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo na mapafu, alianza kusumbuliwa na maradhi hayo karibu mwaka mmoja uliopita.

Kwa mujibu wa mjukuu wa marehemu, Flora Mbasha, baada ya hali yake kutoridhisha, alipelekwa nchini India kwa matibabu zaidi lakini hata aliporudi hali yake haikuwa nzuri.

Kwa mujibu wa ndugu wengine, marehemu Kulola ameishi duniani kwa miaka 85, alizaliwa 1928, Mwanza katika familia yenye watoto kumi, watano wakiwa wameshatangulia mbele ya haki.

WATOTO KUMI.

Marehemu alifunga ndoa na Elizabeth Kulola na kujaliwa kupata watoto kumi, watatu wakiwa wametangulia mbele ya haki.

Uhakika wa idadi ya wajukuu aliowaacha hauko wazi, lakini habari zinasema ameacha wajukuu zaidi ya 45 na vitukuu kibao kwa mkewe Elizabeth.

AANZA KUHUBIRI.

Mwaka 1962 alianza kuhubiri akiwa mfanyakazi wa serikali. Mwaka 1964 ndipo alipoamua kuweka nguvu zake zote katika kumtumikia Mungu huku akiwa anasomea utumishi wa Bwana. 

Mwaka 1966 alimaliza masomo akiwa na stashahada.

AANZISHA MAKANISA ELFU NNE.

Mwaka 1992 ndipo alipoanzisha kanisa la EAGT ambalo lilipata mafanikio makubwa sana katika nchi za Tanzania, Malawi na Zambia na yeye kuwa askofu mkuu akiwa na msaidizi wake, Mwaisabira wakisimamia makanisa elfu nne katika maeneo hayo.

WACHUNGAJI WALIOTOKANA NA YEYE.

Marehemu atakumbukwa kwa kuzalisha  watumshi wengi wa Mungu nchini Tanzania wakiwemo,  Dr. Daniel Moses Kulola (mwanaye), Mchungaji Florian Katunzi, Askofu  Zakaria Kakobe, Antony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’, Dunstan Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

ALIAMURU NYWELE ZAKE ZISIREFUKE.

Katika utumishi wake inadaiwa marehemu hajawahi kwenda saluni kupunguza nywele kwa miaka 47 iliyopita baada ya kuziamuru kwa jina la Yesu zisirefuke.

Aidha vilio vilitawala viwanja vya kanisa la EAGT, Temeke jana(Septemba 2013) wakati mwili wa mwasisi huyo wa makanisa ya kiroho na mhubiri wa kimataifa,  Dk. Moses Kulola, ulipokuwa ukiagwa kwa ajili ya kusafirishwa kwa mazishi yatakayofanyika mkoani Mwanza wiki ijayo.


Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad