Maaskofu na wachungaji wakiwa wamejipanga kuupokea mwili huo wakati ukiwasili viwanja vya kanisa la EAGT, Temeke. |
Mke
wa marehemu, Elizabeth Kulola (wa kwanza kulia) na ndugu wengine (kushoto)
wakilia kwa uchungu.
|
Wajukuu
wa marehemu wakiwa na nyuso za huzuni. Katikati ni mwimbaji wa Injili ambaye ni
mjukuu wa Kulola, Flora Mbasha akilia.
|
Watu
waliohudhuria viwanjani hapo wakilia baada ya mwili kuwasili.
|
Mtumishi wa
Mungu, mchungaji Katunzi akitoa neno fupi na kuombea sadaka.
|
Msemaji wa
Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senso,
akisaini kitabu cha maombolezo.
|
Mchungaji,
Anthony Lusekelo akisaini kitabu cha maombolezo.
|
Mama Getruda
Lwakatare akisaini kitabu cha
maombolezo.
|
…Akisaini kitabu cha maombolezo.
|
Askofu
wa makanisa ya Pentekoste nchini, David Mwasota, akitoa neno la salamu na jinsi
alivyokuwa akimfahamu marehemu Kulola.
|
Mchungaji Josephat Gwajima akitoa salamu za rambirambi. |
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God (EAGT), Moses Kulola amefariki
dunia katika Hospitali ya African
Medical Investment (Ami) iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Marehemu
Kulola aliyefariki dunia saa 5:35 (Agost 29,2013) baada ya kusumbuliwa na
matatizo ya moyo na mapafu, alianza kusumbuliwa na maradhi hayo karibu mwaka
mmoja uliopita.
Kwa
mujibu wa mjukuu wa marehemu, Flora Mbasha, baada ya hali yake kutoridhisha,
alipelekwa nchini India kwa matibabu zaidi lakini hata aliporudi hali yake
haikuwa nzuri.
Kwa
mujibu wa ndugu wengine, marehemu Kulola ameishi duniani kwa miaka 85,
alizaliwa 1928, Mwanza katika familia yenye watoto kumi, watano wakiwa
wameshatangulia mbele ya haki.
WATOTO
KUMI.
Marehemu
alifunga ndoa na Elizabeth Kulola na kujaliwa kupata watoto kumi, watatu wakiwa
wametangulia mbele ya haki.
Uhakika
wa idadi ya wajukuu aliowaacha hauko wazi, lakini habari zinasema ameacha
wajukuu zaidi ya 45 na vitukuu kibao kwa mkewe Elizabeth.
AANZA
KUHUBIRI.
Mwaka
1962 alianza kuhubiri akiwa mfanyakazi wa serikali. Mwaka 1964 ndipo alipoamua
kuweka nguvu zake zote katika kumtumikia Mungu huku akiwa anasomea utumishi wa
Bwana.
Mwaka 1966 alimaliza masomo akiwa na stashahada.
AANZISHA
MAKANISA ELFU NNE.
Mwaka
1992 ndipo alipoanzisha kanisa la EAGT ambalo lilipata mafanikio makubwa sana
katika nchi za Tanzania, Malawi na Zambia na yeye kuwa askofu mkuu akiwa na
msaidizi wake, Mwaisabira wakisimamia makanisa elfu nne katika maeneo hayo.
WACHUNGAJI
WALIOTOKANA NA YEYE.
Marehemu
atakumbukwa kwa kuzalisha watumshi wengi
wa Mungu nchini Tanzania wakiwemo, Dr.
Daniel Moses Kulola (mwanaye), Mchungaji Florian Katunzi, Askofu Zakaria Kakobe, Antony Lusekelo ‘Mzee wa
Upako’, Dunstan Maboya, Mwasota na wengineo wengi.
ALIAMURU
NYWELE ZAKE ZISIREFUKE.
Katika
utumishi wake inadaiwa marehemu hajawahi kwenda saluni kupunguza nywele kwa
miaka 47 iliyopita baada ya kuziamuru kwa jina la Yesu zisirefuke.
Aidha
vilio vilitawala viwanja vya kanisa la EAGT, Temeke jana(Septemba 2013) wakati
mwili wa mwasisi huyo wa makanisa ya kiroho na mhubiri wa kimataifa, Dk. Moses Kulola, ulipokuwa ukiagwa kwa ajili
ya kusafirishwa kwa mazishi yatakayofanyika mkoani Mwanza wiki ijayo.
Bwana
ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina.
No comments:
Post a Comment