![]() |
Wanajeshi wa
DRC washerekea ushindi dhidi ya M23 Katika eneo la Kibati.
|
![]() |
Wanajeshi wa
DRC wakitembea Kibati baada ya kuwarudisha nuyuma M23.
|
![]() |
Mnara wa
mawasiliano uloharibiwa katika ene la Kibati DRC.
|
![]() |
Ngome iliyotekekezwa ya M23 eneo la Kibati. |
![]() |
Picha ya Gari la kundi la M23 lililoharibiwa na majeshi ya DRC. |
Kundi la M23
la jamhuri ya kidemokrasi ya kongo linasema linasitisha mapigano na jeshi la
Congo na kuondoka kwenye eneo ambalo mapigano yalikuwa makali katika siku za
karibuni ili kuruhusu uchunguzi huru ufanyikwe kuhusiana na mizinga
iliyoshambulia Rwanda .
Nchi ya
Rwanda wiki hii imeyatuhumu majeshi ya
serikali ya Congo kwa kufyatua mizinga na roketi ndani ya ardhi yake , lakini
umoja wa mataifa na serikali ya Kigali wanalilaumu kundi la M23 kwa mashambulio
hayo.
Kiongozi wa
kundi la M23 Bw.Bertrand Bisimwa
aliiambia Sauti ya America - VOA kwamba
wapiganaji wake wanaondoka kwenye maeneo yao katika kijiji cha Kanyaruchinya ,
karibu na Goma kwenye mpaka wa Congo na Rwanda ili kuruhusu uchunguzi ufanyike kuamua nani hasa alihusika.
Naye msemaji
wa majeshi ya serikali FARDC Olivia
Amuli akizungumza na Sauti ya Marekani
VOA anasema kwamba wanajeshi wa serikali
wamerudisha nyuma wapiganaji wa M23 na M23 wameondoka kwasababu ya kupata pigo
kubwa aliongeza kuwa baada ya mapambano ya siku 9 hatimaye wamedhibiti
maeneo ya Kibati na Kilimanyoka
na kusema waasi hao wamekimbia huku wakiwa wameacha magari yao yaliopigwa na
mabomu.
Wakati huo
huo Nchi ya Rwanda imekanusha madai kuwa wanajeshi wake wapo tayari kupambana
na majirani zao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, taarifa hizo zilienea
baada ya kushuhudiwa msafara wa wanajeshi na magari ya silaha kutokea mjini
Kigali kuelekea eneo la mpakani na DRCongo.
Waziri wa
nchi za nje wa Rwanda Bi.Louise
Mushikiwabo alisema vikosi vya nchi yake havijaingia DRC na andapo uamuzi huo
utachukuliwa basi taarifa zitawekwa wazi, taarifa hiyo ameitoa kupitia mtandai
wa kijamii wa twitter.
Jeshi la
serikali FRDC wakishirikiana na vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyolinda amani
nchini DRCongo na upande wa pili wa waasi wa M23 wamekuwa wakishutumiana kila
mmoja akimtaja mwenzie kuhusika na shambulizi hilo.
Chanzo:VOA
No comments:
Post a Comment