Picha za Muonekano wa Majeshi ya serikali ya Congo yawarudisha nyuma wapiganaji wa M23. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 31, 2013

Picha za Muonekano wa Majeshi ya serikali ya Congo yawarudisha nyuma wapiganaji wa M23.

Wapiganaji wa M23 walitangaza ijumaa kwamba wanaondoka kutoka mstari wa mbele wa mapigano na majeshi ya serikali ya Congo.
 Lakini maafisa wa serikali wanasema M23 wameshindwa katika mapigano karibu na Goma-Picha na VOA.


Wanajeshi wa DRC washerekea ushindi dhidi ya M23 Katika eneo la Kibati.

Wanajeshi wa DRC wakitembea Kibati baada ya kuwarudisha nuyuma M23.

Mnara wa mawasiliano uloharibiwa katika ene la Kibati DRC.

Ngome iliyotekekezwa ya M23  eneo la  Kibati.

Picha ya Gari la kundi la M23 lililoharibiwa na majeshi ya DRC.


Kundi la M23 la jamhuri ya kidemokrasi ya kongo linasema linasitisha mapigano na jeshi la Congo na kuondoka kwenye eneo ambalo mapigano yalikuwa makali katika siku za karibuni ili kuruhusu uchunguzi huru ufanyikwe kuhusiana na mizinga iliyoshambulia Rwanda .

Nchi ya Rwanda  wiki hii imeyatuhumu majeshi ya serikali ya Congo kwa kufyatua mizinga na roketi ndani ya ardhi yake , lakini umoja wa mataifa na serikali ya Kigali wanalilaumu kundi la M23 kwa mashambulio hayo.

Kiongozi wa kundi la M23  Bw.Bertrand Bisimwa aliiambia Sauti ya America - VOA  kwamba wapiganaji wake wanaondoka kwenye maeneo yao katika kijiji cha Kanyaruchinya , karibu na Goma kwenye mpaka wa Congo na Rwanda ili kuruhusu uchunguzi ufanyike  kuamua nani hasa alihusika.

Naye msemaji wa majeshi ya serikali FARDC  Olivia Amuli  akizungumza na Sauti ya Marekani VOA  anasema kwamba wanajeshi wa serikali wamerudisha nyuma wapiganaji wa M23 na M23 wameondoka kwasababu ya kupata pigo kubwa aliongeza kuwa baada ya mapambano ya siku 9 hatimaye  wamedhibiti  maeneo ya Kibati  na Kilimanyoka na kusema waasi hao wamekimbia huku wakiwa wameacha magari yao yaliopigwa na mabomu.

Wakati huo huo Nchi ya Rwanda imekanusha madai kuwa wanajeshi wake wapo tayari kupambana na majirani zao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, taarifa hizo zilienea baada ya kushuhudiwa msafara wa wanajeshi na magari ya silaha kutokea mjini Kigali kuelekea eneo la mpakani na DRCongo.

Waziri wa nchi za nje wa Rwanda  Bi.Louise Mushikiwabo alisema vikosi vya nchi yake havijaingia DRC na andapo uamuzi huo utachukuliwa basi taarifa zitawekwa wazi, taarifa hiyo ameitoa kupitia mtandai wa kijamii wa twitter.

Jeshi la serikali FRDC wakishirikiana na vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyolinda amani nchini DRCongo na upande wa pili wa waasi wa M23 wamekuwa wakishutumiana kila mmoja akimtaja mwenzie kuhusika na shambulizi hilo.

Chanzo:VOA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad