BONDIA
Mtanzania, Francis ‘SMG’ Cheka Jana (Agosti 30,2013) usiku wa kuamkia leo ametawazwa kuwa bingwa mpya
wa dunia wa WBF, katika uzito wa Super Middle baada ya kumshinda Mmarekani,
Phil Williams kwa pointi katika pambano la Raundi 12, lililofanyika kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Jaji
wa kwanza Eddie Marshall kutoka Afrika Kusini alitoa pointi 116 kwa 115, jaji
wa pili Fidel Hayness alitoa pointi 119 kwa 118 na jaji wa tatu, John Chagu
alitoa pointi 117 kwa 116 (wote wa Tanzania), wakimpa ushindi Cheka.
Kwa
ushindi huo, Cheka amefuata nyayo za bondia mwingine Mtanzania, Rodgers ‘Tiger’
Mtagwa ambaye aliwapiga Wamarekani kadhaa kwao, ambako anaishi tangu 1998.
Miongoni
mwa mabondia Wamarekani ambao Mtagwa, mtoto wa Keko Mwanga, Temeke, Dar es
Salaam amewahi kuwapiga ni Garvin Crout kwa Knockout (KO) Raundi ya kwanza
pambano la Raundi nane, kwenye ukumbi wa Blue Horizon, Philadelphia,
Pennsylvania, Marekani pambano lililochezeshwa na refa James Condon Septemba
12, mwaka 2000 na mwingine Donovan Carey kwa KO pia Raundi ya Pili Juni 15,
2001 ukumbi huo huo.
Katika
pambano hilo lililochezeshwa na refa kutoka Afrika Kusini, Drake Ribbinck,
mabondia hao walianza kwa kusomana Raundi ya kwanza wakitupiana makonde ya
tahadhari na katika Raundi ya pili, kila mmoja alitaka.
Cheka
aling’ara katika Raundi ya Tatu na ya nne na Mmarekani akaibuka Raundi ya Tano
na kuanza kuonyesha upinzani. Raundi ya Sita Mmarekani aliongeza kasi ya
urushaji makonde na Raundi ya saba na ya nane walipigana sawa, ingawa Williams
alianguka kwa kuteleza na kuinuka kuendelea na pambano.
Raundi
ya 10 mabondia hao waliendelea kutupiana makonde kwa zamu, lakini Raundi ya 11
na 12 pamoja na Williams kusimama imara kutafuta ushindi wa Knockout (KO),
lakini SMG alikuwa makini katika kukwepa na kurusha ngumi za kudonoa kichwani
kwa mpinzani wake.
Na
kwa sababu hiyo haikushangaza baada ya pambano, bondia mwenye maskani yake
Morogoro kutangazwa bingwa mpya wa WBF.
Waziri
wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara aliyekuwa mgeni
rasmi alijaribu kwa tabu tabu kumvisha taji Cheka kutokana ulingo kuvamiwa na
mashabiki waliopagawa na ushindi wa bondia huyo.
Katika
mapambano ya utangulizi, Thomas Mashali alimshinda kwa pointi Mada Maugo,
wakati Alphonce Mchumia Tumbo alimshinda kwa Technincal Knockout (TKO), baada
ya wasaidizi wake kurusha taulo Raundi ya tano katika pambano la Raundi sita.
Hata
hivyo, dosari iliyojitokeza katika usiku
huo ni mabondia kugoma kupanda ulingoni hadi kwanza walipwe fedha zao na
ilianzia kwa Mchumia Tumbo, ikafuatia kwa Maugo na Mashali na baadaye Cheka.
No comments:
Post a Comment