Taswira ya Ligi Kuu Uingereza: Arsenal wakiendeleza Rekodi yao ya kutofungwa Nyumbani huku Liverpool ikishinda Mechi ya tatu mfululizo dhidi ya Mabingwa Manchester United. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 02, 2013

Taswira ya Ligi Kuu Uingereza: Arsenal wakiendeleza Rekodi yao ya kutofungwa Nyumbani huku Liverpool ikishinda Mechi ya tatu mfululizo dhidi ya Mabingwa Manchester United.

ANFIELD.
Katika Dimba la ANFIELD  jana Jumapili(Septemba 01,2013) ilishuhudia Liverpool ikishinda Bao   1-0 katika Mechi ya tatu mfululizo ya Ligi Kuu Uingereza huku Mfungaji katika Mechi zote akiwa ni yule yule Daniel Sturridge aliefunga Bao katika Dakika ya 4 tu na kuwaangusha Mabingwa watetezi wa  Uingereza  Manchester United.

Aidha (Septemba 01) ni Bethdei ya Sturridge na  Liverpool ndio wametimiza mwanzo wao mzuri kabisa katika Ligi kwa Miaka 19 na kuwafanya wawe kileleni mwa Ligi wakiwa na Pointi 9 kwa Mechi 3.

Bao la Liverpool lilifungwa kufuatia Kona ambayo Beki wao Agger alipiga kichwa na Mfungaji Sturridge kuuparaza Mpira wavuni.

Kwa Man United, hii ikiwa Mechi yao ya 3 ya Ligi, wana Pointi 4 baada ya kushinda moja, sare moja na kufungwa moja huku katika mchezo huo  Man United walipata nafasi kadhaa zikiwemo zile za Nani na Robin van Persie.

Sturridge akiunanisha pasi ya Daniel Agger na ameifungia Liverpool katika mechi zote tatu msimu huu katika Ligi Kuu ya England, baada ya kuifunga Manchester United 1-0 Anfield.



Sturridge akimkumbatia kocha wake Brendan Rodgers baada ya kufunga bao muhimu kwa Liverpool.


Gerrard akipiga shuti la mpira wa adhabu ambalo liliokolewa na kipa David de Gea wakati wa mchezo huo.

Steven Gerrard na Robin van Persie wakichimbiana mikwara wakati wa mchezo huo.

Danny Welbeck akienda chini baada ya kuchezewa rafu na Lucas na Iago Aspas

Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez anayetumikia adhabu alikuwepo Jukwaani akifatilia mchezo huo ambao Liverpool walishinda bao 1-0 dhidi ya Manchester United.

Makocha: Kocha wa Liverpool, Rodgers (kulia) na wa Manchester United, David Moyes wakiwa kazini katika mchezo huo.

Man United walicheza Mechi hii bila ya Nyota wao Wayne Rooney ambae  Mazoezini alipasuka Paji la Uso baada ya kugongana na mwenziwe na inasemekana ameshonwa Nyuzi 10.

Arsenal .
Nao Arsenal wameendeleza Rekodi yao murua ya kutofungwa Nyumbani na Mahasimu wao wa London ya Kaskazini, Tottenham, baada ya  kuwachapa Bao 1-0 katika Mechi ya Ligi Kuu na hivyo kudumisha Rekodi ya kufungwa nao  mara moja tu tangu Mwaka 1993.

Tottenham ilipokea kipigo chao cha kwanza cha Ligi Msimu huu kwa Bao la Dakika ya 23 la Olivier Giroud baada kuunganisha krosi ya chini ya Theo Walcott na hilo ni Bao lake la 4 Msimu huu.

Olivier Giroud ameifungia bao pekee Asrenal leo Emirates


Ushindi huu umewafanya Arsenal wakamate Nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi baada ya kila Timu kucheza Mechi 3 na kuhakikisha Tottenham wameshinda mara moja toka 1993 Nyumbani kwa Arsenal.

LIGI KUU ENGLAND RATIBA 2013/2014.

Jumamosi 14 Septemba,2013.

14:45 Manchester United v Crystal Palace

17:00 Aston Villa v Newcastle United

17:00 Fulham v West Bromwich Albion

17:00 Hull City v Cardiff City

17:00 Stoke City v Manchester City

17:00 Sunderland v Arsenal

17:00 Tottenham Hotspur v Norwich City

19:30 Everton v Chelsea


Jumapili 15 Septemba,2013.

18:00 Southampton v West Ham United

Jumatatu 16 Septemba,2013.


22:00 Swansea City v Liverpool

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad