KOCHA Mkuu
wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen ameita kambini
wachezaji 24 kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia
itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
Wachezaji
hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili
usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa
kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.
Makipa
walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Huru), Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa
(Yanga) na Aishi Manula (Azam).
Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani
(Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam),
Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David Luhende (Yanga).
Viungo ni Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank
Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amri Kiemba
(Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Bocco (Azam), Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Mbwana Samatta (TP
Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
Wakati huo
huo; Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Taifa Stars, Baraka Kitenge (74)
kilichotokea leo mchana (Agosti 20 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Msiba huo ni
mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Kitenge akiwa
mchezaji, alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea, hivyo mchango
wake tutaukumbuka daima.
Kitenge
amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa akisumbuliwa
na kansa ya uti wa mgongo. Enzi zake katika Yanga na Taifa Stas alicheza na
wachezaji kama akina Athuman Kilambo na Abdulrahman Juma.
TFF imetoa
pole kwa familia ya marehemu Kitenge, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mipango ya
mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu, Yombo Vituka (Jet) jijini Dar es
Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Kitenge mahali pema peponi. Amina
No comments:
Post a Comment