 |
Viongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema ,Mwenyekiti wa Chadema Bw Freeman Mbowe, Mkurugenzi
wa Habari na Uenezi wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Bw John Mnyika na
Bw.Tundu Lisu wakijiandaa kutua katika uwanja wa posta ya zamani Mjini Ngara (Agost
17,2013) kushiriki mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa
wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,lililoandaliwa na chama hicho.
|
 |
Toka kushoto ni Mbunge Anton Mbasa,Mwenyekiti wa Chadema Bw Freeman Mbowe, Mkurugenzi
wa Habari na Uenezi wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Bw John Mnyika wakiondoka katika uwanja wa posta ya zamani Mjini Ngara (Agost
17,2013) baada ya kumalizika mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa
wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,lililoandaliwa na chama hicho.
|
 |
Muonekano wa Wanachama wapya wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema waliojiunga ,wakitoka Vyamba vya CCM na NCCR-Mageuzi na kukabidhiwa Kadi na Mwenyekiti wa Chadema Bw Freeman Mbowe, wakati wa mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa
wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,lililoandaliwa na chama hicho.
|
 |
Gari la Radio Kwizera lenye Matangazo ya Nje PA (Lililokodiwa na Chadema) likiendelea na Matangazo yake uwanjani hapo katika mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa
wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera, (Kwa mahitaji ya Matangazo na Vifaa Vyake fika Ofisi za radio Kwizera-Ngara) upate kwa bei nafuu kabisa kwa ajili ya sherehe na Mikutano ya Vyama mbalimbali vya Siasa).
|
 |
Wananchi ,Wapenzi na Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)wakipitisha maoni yao wakati wa mkutano wa baraza huru la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa
wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,lililoandaliwa na chama hicho(Agosti 17,2013).
|
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema kimetoa wito kwa Watanzania kuunga mkono rasimu ya katiba
mpya iliyoratibiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Mstaafu Joseph
Warioba.
Mwenyekiti wa Chadema Bw
Freeman Mbowe alitoa wito huo (Agost 17,2013) wakati wa mkutano wa baraza huru
la wazi la Katiba ya Chama hicho kwa wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani
Kagera,lililoandaliwa na chama hicho.
Bw.Mbowe alisema kwa asilimia
kubwa rasimu ya katiba inayoendelea kujadiliwa imezingatia mambo makuu ya
kitaifa hasa muundo wa serikali kwa kupendekeza kuwepo na serikali 3.
Aidha Mwenyekiti huyo Taifa
wa CHADEMA amewataka Watanzania kuhakikisha Kiswahili kinakuwa Lugha rasmi ya
Taifa katika katiba ijayo na kwamba Kiingereza linapaswa kuwa somo la lazima
kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu ili kuwaandaa kwa usawa Watanzania
wote katika ushindani wa ajira baada ya kuhitimu masomo yao.
Nae mkurugenzi wa Habari na
Uenezi wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Bw John Mnyika ameitaka Wizara
ya Katiba na Sheria kuhakikisha inachapisha na kusambaza nakala za Rasimu ya
Katiba mpya nchini Kote ili Watanzania waisome na kutoa maoni sahihi ili kupata
Katiba bora.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi
wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera waliotoa maoni yao mbele ya viongozi hao wa
Chadema wamependekeza kuwa Katiba ijayo itamke bayana kuhusu haki ya Demokrasia
ya Vyama vingi,Utawala wa Sheria na Haki za Binadamu pamoja na Wananchi
kumiliki Rasilimali na Maliasili za taifa na Kunufaika nazo.
No comments:
Post a Comment