Cheki Picha na Matokeo ya Mechi ya Chelsea,FC Barcelona na Arsenal Jana Agosti 21,2013. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 22, 2013

Cheki Picha na Matokeo ya Mechi ya Chelsea,FC Barcelona na Arsenal Jana Agosti 21,2013.

Chelsea wakishangilia baada ya kushinda 2-1 baada ya Branislav Ivanovic Jana(Agosti 21,2013) Usiku alifunga Bao la Pili la kichwa na la ushindi na kuipa Chelsea pointi 3 muhimu dhidi ya Aston Villa katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Stamford Bridge.


Branislav Ivanovic  akifunga bo la ushindi dakika ya 73 ya mchezo huo.

Jose Mourinho akizinguana na kocha mpinzani wake, Paul Lambert na Ugomvi  huo ulitokana na rafu ya Ivanovic kwa Christian Benteke huku Refa wa akiba akijaribu kuwasuluhisha.

-Christia Benteke  akishangilia bao lake alilofunga dakika ya 45.


Branislav Ivanovic Jana(Agosti 21,2013) Usiku alifunga Bao la Pili la kichwa na la ushindi na kuipa Chelsea ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Aston Villa katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Stamford Bridge lakini Meneja wa Aston Villa, Paul Lambert, amelalamika kuhusu uamuzi wa matukio mawili muhimu kwenye Mechi hiyo.

Chelsea walipata Bao la kwanza baada ya shuti la Eden Hazard kuokolewa na Kipa Guzan na kumgonga Beki Antonio Luna na kutinga wavuni dakika ya 6 ya mchezo huo.

Christian Benteke alisawazisha kwa Aston Villa dakika ya 45 lakini Ivanovic ndio aliwapa ushindi Chelsea dakika ya 73 ya mtanange huo.

Matukio ambayo Aston Villa wamelalamika ni yale ya Dakika ya 69 wakati Branislav Ivanovic alipopewa Kadi ya Njano kwa kumpiga kipepsi Christian Benteke badala ya Kadi Nyekundu na tukio la Dakika za nyongeza wakati John Terry alipounawa Mpira wa Kichwa cha Gabriel Agbonlahor.

Hii ni Mechi ya Pili kwa Chelsea kushinda baada ya kuifunga Hull City Bao 2-0 katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Jumapili iliyopita.


RATIBA IJAYO YA LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi 24 Agosti,2013.


14:45 Fulham v Arsenal

17:00 Everton v West Bromwich Albion

17:00 Hull City v Norwich City

17:00 Newcastle United vWest Ham United

17:00 Southampton v Sunderland

17:00 Stoke City v Crystal Palace

19:30 Aston Villa v Liverpool

Jumapili 25 Agosti,2013.


18:00 Cardiff City v Manchester City

18:00 Tottenham Hotspur v Swansea City


Jumatatu 26 Agosti,2013.


22:00 Manchester United v Chelsea


David Villa akishangilia baada ya kuifunga timu yake ya zamani FC Barcelona , aliifungia dakika ya 12  Atletico Madrid.


Katika uwanja wa ESTADIO VICENTE CALDERON Jana(Agosti 21,2013) Usiku ilishuhudia Wachezaji wapya kwa Timu zao wakifunga Bao katika Mechi ya kwanza ya kugombea Supercopa De Espana ambapo Atletico Madrid na Barcelona zilitoka sare Bao 1-1.

Timu hizi zitarudiana huko Nou Camp Jumatano ijayo.

Bao la Atletico Madrid lilifungwa katika Dakika ya 12 na David Villa Mchezaji ambae alihamia Atletico akitokea Barca Mwezi uliopita.

Barcelona walisawazisha kwa Bao la Neymar alieingizwa katika Dakika ya 59 na kufunga Bao hilo katika Dakika ya 66 na hilo ni Bao lake la kwanza kwa Barca katika Mashindano rasmi.

Katika Mechi hii Barca walilazimka kumpumzisha Lionel Messi wakati wa Mapumziko kutokana na maumivu na nafasi yake kuchukuliwa na Cesc Fabregas.


Neymar akishangilia kuifungia klabu yake mpya, Barcelona aliyojiunga nayo kutoka kwa dau la Pauni Milioni 48.

Lionel Messi alitolewa nje baada ya kuumia katika mchezo huo wa Super Cup jana na Messi alikosa mechi kadhaa mwishoni mwa msimu uliopita kwa maumivu ya nyama mguu wa kulia.

(Kutoka kushoto) Carl Jenkinson, Kieran Gibbs, Theo Walcott, Aaron Ramsey na Olivier Giroud wakishangilia bao la kwanza la -Kieran Gibbs aliloifungia Arsenal Dakika ya 51.

Olivier Giroud akiifungia Arsenal bao la tatu kwa penalti baada ya Theo Walcott kuchezewa rafu na Michal Kadlec kwenye boksi.

Aaron Ramsey akiifungia Arsenal bao la pili katika Dakika ya 64 ya mchezo huo muhimu sana .


Wakicheza Ugenini huko Sukru Saracoglu Stadium Mjini, İstanbul, Nchini Uturuki dhidi ya Fenerbahce katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONSZ LEAGUE, Arsenal wameibuka na ushindi mnono wa Bao 3-0.

Arsenal waliingia kwenye Mechi hii wakitoka kwenye kipigo cha Bao 3-1 katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England walipochapwa na Aston Villa tena kwao Uwanja wa Emirates Jumamosi iliyopita.

Lakini Bao 3 za Kipindi cha Pili zimewafanya wawe katika hali nzuri kwa ajili ya Mechi ya Marudiano itakayochezwa Emirates Jumanne ijayo.

Pamoja na Mechi ya Arsenal, pia hiyo Jana kulikuwa na Mechi nyingine 4 za kwanza za Raundi ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

Washindi wa Raundi hii wanaingia hatua ya Makundi.


MATOKEO:-UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MCHUJO-RATIBA:-Jumanne Agosti 20,2013.

Shakhter Karagandy 2 Celtic 0

Lyon 0 Real Sociedad 2

Pacos de Ferreira 1 Zenit St Petersburg 4

Viktoria Plzen 3 NK Maribor 1

PSV Eindhoven 1 AC Milan 1

Marudiano Agosi 27 na 28,2013.

jumatano Agosti 21,2013.

Fenerbahce 0 Arsenal 3

Schalke 1 PAOK Salonika 1
 
Steaua Bucharest 1 Legia Warsaw 1

Ludogorets Razgrad 2 FC Basel 4

Dinamo Zagreb 0 Austria Wien 2


***FAHAMU: Washindi 10 wa hii Raundi ya Mchujo wataingia Hatua ya Makundi ambapo watajumuika na Timu 22 zinazoingia moja kwa moja.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad