Ajali mbaya ya Basi yaua watu 37 Nchini Malaysia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET

Post Top Ad

Friday, August 23, 2013

Ajali mbaya ya Basi yaua watu 37 Nchini Malaysia.

Takribani watu 37 wameripotiwa kupoteza maisha Mjini  Kuala Lumpur nchini Malaysia ,baada ya basi walilopanda kutumbukia katika korongo refu.

Maafisa wa usalama nchini humo wamesema ajali hii ni moja ya ajali kubwa ambazo zimewahi kutokea, kutokana na kusababisha vifo vya watu wengi.

Baadhi ya abiria wameokolewa kutoka katika korongo hilo ambalo lina urefu wa futi 200 hali iliyosababisha waokoaji kutumia cranes pamoja na kamba kuweza kuokoa majeruhi wa ajali hiyo.

Ripoti  zinasema kwamba basi hilo lilibeba abiria wapatao 49 na mpaka sasa ni abiria 16  waliokolewa wakiwa hai japokuwa hali zao bado ni mbaya na huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Licha ya kutokea ajali iyo maafisa wa usalama wameshindwa kutambua uraia wa wahanga wa ajali iyo.

Baadhi ya abiria wameokolewa kutoka katika korongo hilo ambalo lina urefu wa futi 200 hali iliyosababisha waokoaji kutumia cranes pamoja na kamba kuweza kuokoa majeruhi wa ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad