Taswira ya Kuapishwa Rais Robert Mugabe kwa muhula mwingine wa Saba mbele ya halaiki ya watu wakishiriki. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 23, 2013

Taswira ya Kuapishwa Rais Robert Mugabe kwa muhula mwingine wa Saba mbele ya halaiki ya watu wakishiriki.




Rais wa Zimbabwe Comrade Robert Gabriel Mugabe amekula kiapo cha kuitumikia nchi hiyo kwa muhula wa 7 mfululizo katika sherehe zilizofanyika mjini Harare, August 22, 2013.



Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ashika bibilia akila kiapo wakati wa sherehe za kuapishwa kwake mjini Harare na ameahidi "kuilinda na kuitetea katiba ya Zimbabwe".


Rais Robert Mugabe na mkewe Grace waikiwapungia mkono umati wa watu alipokuwa anawasili kwenye uwanja wa michezo kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake mjini Harare, August 22, 2013.


A supporter of Zimbabwean President Robert Mugabe attends his inauguration in Harare, August 22, 2013.


Mfuasi wa rais Robert Mugabe akibeba bango la rais wakati wa sherehe za kuapishwa kwake mjini Harare, August 22, 2013.

Rais wa Zimbabwe Comrade Robert Gabriel Mugabe amekula kiapo cha kuitumikia nchi hiyo kwa muhula wa 7 mfululizo katika sherehe zilizofanyika mjini Harare.

Katika kiapo mbele ya Jaji Mkuu Godfrey Chidyausiku maelfu ya wafuasi wake, Mugabe ameahidi "kuilinda na kuitetea katiba ya Zimbabwe".

Wakuu wa nchi 40 walikuwa wamealikwa katika sherehe hizo, ambazo zimesusiwa na upinzani.

Msemaji wa kiongozi wa upinzani nchini humo, Morgan Tsvangirai, alisema kiongozi huyo hawezi kushiriki katika kile alichokiita 'sherehe ya mwizi'.

Tofauti na sherehe zilizopita kumwapisha Mugabe ambazo hazikuwa na shamrashamra, hii ya mwaka huu imepewa umuhimu mkubwa ambapo Maelfu ya raia wapatao elfu 60 walihudhuria sherehe hizo ambazo pia viongozi mbalimbali wa bara la Afrika walialikwa.

Sherehe hizo zimefanyika baada ya mahakama kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na upinzani kupinga matokeo hayo na kumtangaza rais Mugabe kama mshindi halali huku pia viongozi wa MDC wakiwa hawajaalikwa kwenye sherehe hizo.

Ma rais kadhaa wa bara la Afrika tayari wamewasili jijini Harare kuhudhuria katika sherehe hizo.

Hivi majuzi viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika SADC waliitaka jamii ya kimataifa kuiondolea vikwazo Zimbabwe, baada ya uchaguzi kufanyika katika hali tulivu.

Marekani tayari imetangaza kuindolea vikwazo Zimbabwe pale tu rasi mugabe atakuwa tayari kufanya mageuzi kwa mujibu wa matakwa ya wananchi wake.

Rais Mugabe anatimiza mwaka wa 33 madarakani na kuwa mmoja kati ya viongozi wa Bara la Afrika aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi huku mwenyewe akitamba kutaka kuongoza taifa hilo mpaka atakapofikisha umri wa miaka 100.


Hivi sasa rais Mugabe ana umri wa miaka 89 na ameapishwa kwa ajili ya muhula mwengine wa miaka mitano kuliongoza taifa hilo la Zimbabwe na wachambuzi wanaonya kuwa amri ya mahakama hiyo kutupilia mbali madai ya Tsvangirai aliyepinga matokeo ya uchaguzi ni kichocheo cha ukandamizaji wa kisiasa.

Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe ilitangaza kuwa chama cha ZANU-PF kilishinda theluthi tatu ya idadi ya viti bungeni na kwamba Mugabe alipata ushindi wa zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizopigwa.
Lakini wiki iliyopita Tsavangirai alifutilia mbali madai yake dhidi ya ZANU-PF, baada ya kuyapeleka katika Mahakama Kuu kupinga matokeo ya uchaguzi, akisema hana imani ya kupata haki mahakamani huko. Siku ya Jumanne mahakama hiyo ilisema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki na kuwa ulizingatia matakwa ya raia wake.
Tsvangirai anadai kuwa takribani wapiga kura milioni moja waliondolewa kwenye vituo vya kupigia kura katika maeneo ya mijini yanayoaminiwa kuwa ni ngome yake ya kisiasa, ingawa mahakama ilifutilia mbali madai hayo.
Hata hivyo, msemaji wa Tsvangirai, Douglas Mwonzora, ameiambia IPS kuwa hakushangazwa na uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo, kwa kuwa walilijua suala hilo mapema.
Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mugabe zilikuwa zimecheleweshwa kufanyika kutokana na kesi hiyo.


Source:DW. 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad