![]() |
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk
Shukuru Kawambwa.
|
Baraza la
mitihani Tanzania NECTA limetangaza rasmi matokeo ya Kidato cha Nne 2012.
Idadi
ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa
kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya
marekebisho alama za viwango vya ufaulu.
Matokeo hayo
mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne
umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda
yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao
awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata
madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo
hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011,
ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani
huo walifaulu.
Matokeo ya
awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru
Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa
kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la
tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni
103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika
matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu
ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata
daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
KUPATA
MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE 2012 BOFYA HAPA:-http://www.necta.go.tz/matokeo_html_2013/CSEE_2012/olevel.htm
No comments:
Post a Comment