Happy Muungano Day,Miaka 49 na askari 30 wakitunukiwa nishani mbalimbali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Rais Jakaya Kikwete. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 27, 2013

Happy Muungano Day,Miaka 49 na askari 30 wakitunukiwa nishani mbalimbali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Rais Jakaya Kikwete.


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo kuongoza Watanzania kusherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Pamoja naye kwenye gari hilo la wazi ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange



Aidha Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa msamaha kwa wafungwa 4,180 ,ili waende kuungana na familia zao,na kwamba watakuwa wamepata fundisho na wataishi vyema kwenye jamii walizotoka.




Aidha msamaha huo haukuwausu waenye kifungo cha maisha, watumiaji madawa ya kulevya.


Msafara wa Rais Kikwete ukizunguka uwanja wa Uhuru




Na ndege za mafunzo za kivita zilionyesha umahili uliyotumika na marubani wa ndege hizo,ambapo ndege ya tano iliendeshwa na Luteni Kanali Sinzia.



Taswira maonyesho ya Ndege za kijeshi kwenye sherehe za miaka 49 ya Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar  leo(April 26,2013).


Maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilijumuisha Gwaride lilokuwa na Guard 10, ambazo zilikaguliwa na Rais.


Pia kukawa na watoto wa halaiki 2,695 wa kutoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani ambao walinyesha mazoezi ya viungo,kutengeneza maumbo mbalimbali yenye mafundisho.Na wazheza sarakasi 35 ambao walionyesha michezo kadhaa matika kustarehesha wananchi waliyofurika uwanja wa Uhuru.




Sherehe hizo zilipambwa na ngoma kutoka Tarime Mkoa wa Mara,Gonga kutoka Mkoa wa Kusini Pemba na Sindimba kutoka Mkoa wa Lindi na kwaya kutoka JKT  Masange  Tabora. 


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii.


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku Meja Jenerali wa JWTZ, Protest Rwegasira Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii.


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku Kanali Shaban Lissu Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii.


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku Meja Janeth Izengo Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii.


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku Naibu Kamisna wa Polisi, Suleiman Kova Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii.


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku SACP Adolphina Chialo Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii.


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku Kamishna wa Magereza Dionice Chamulesie Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii.


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku Kamishna wa Magereza  Juma  Malewa Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunukuACP Sania Kigwe Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii.


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku Kanali Adolph Mutta wa JWTZ, Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzania, katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)


Amir Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimtunuku Luteni Kanali Michael Mumanga wa Kikosi cha Maji cha JWTZ, Niashani ya Utumishi wa Mrefu Tanzania,  katika hafla ya kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jioni hii


Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Rais Jakaya Kikwete (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na askari 30 aliowatunuku nishani mbalimbali, ikiwa ni moja ya shamrashamra ya kuadhimiasha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Ikulu, Dar es Salaam leo.  (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad