Kuanzia sasa kazi ya kuandikisha wanafunzi kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, itafanywa na watendaji wa vijiji na si Walimu wakuu wa shule za Msingi Nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 21, 2013

Kuanzia sasa kazi ya kuandikisha wanafunzi kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, itafanywa na watendaji wa vijiji na si Walimu wakuu wa shule za Msingi Nchini.



Naibu Waziri wa Elimu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassimu Majaliwa, amesema kuanzia sasa kazi ya kuandikisha wanafunzi kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, itafanywa na watendaji wa vijiji na si walimu wakuu wa shule za msingi.




Majaliwa aliyasema hayo juzi, wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari na baadhi ya viongozi wa sekta ya elimu mkoani hapa,katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.



Alisema watendaji wa vijiji ndio wanawafahamu zaidi watoto wanaostahili kuanza elimu ya awali na msingi  kuliko walimu wakuu wa shule za msingi katika maeneo husika.



Alisema kutokana na ukweli huo, kazi ya uandikishaji watoto wenye sifa ya kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, ni watendaji wa vijiji na kazi hiyo,itakuwa na ufanisi mkubwa kuliko kipindi cha miaka ya nyuma.



“Kwa hiyo, kuanzia sasa kazi ya kuanza kuandikisha wanafunzi wa madarasa ya awali na ya msingi, itaanza mapema mara tu shule zitakapofunguliwa Januari na hadi kufikia Agosti ya mwaka husika, kazi hiyo itakuwa imekamilika.Kwa sasa hatutasubiri hadi mwishoni mwa mwaka kuandikisha wanafunzi”, alifafanua Majaliwa.



Aidha, Naibu Waziri huyo, alisema kuwa kila mtendaji wa kijiji, anapaswa kuwakilisha ripoti ya kazi ya uandikishaji wanafunzi wa shule za awali na wale wa msingi mbele ya Kikao cha Maendeleo ya Kata (WDC),ili kupata Baraka ya kikao hicho.



Alisema ili kuipa umuhimu mkubwa elimu ya awali, ni lazima kuwepo na bajeti ambazo zitaonyesha ongezeko la shule za awali.



Katika hatuna nyingine, Naibu waziri huyo alikumbusha kuwa kila shule ya msingi, ni lazima iwe na vyumba vya kutosha vya madarasa ya awali. 



Wanafunzi wa shule za awali sio walundikwe tu madarasa au wawe wa kucheza tu kipindi chote wawapo shuleni, hapana, ihakikishwe wanasoma kikamilifu ili wakianza darasa la kwanza katika shule za msingi, wawe wameiva barabara,” alisema Majaliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad