![]() |
|
Dr.Hussein
Mwinyi.
|
Utafiti wa
Kitaifa wa Afya uliofanywa mwaka 2010 umeonyesha kuwa asilimia 72 ya wanawake
na watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa
nafasi ya pili kwa kuwa na asilimia 46 ambayo ni zaidi na kiwango cha ukatili
huo nchi nzima ambacho ni asilimia 44.
Kwa mujibu
wa utafiti huo ambao ulifanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii umeonyesha
kuwa Mkoa wa Tanga una idadi ndogo ya vitendo hivyo ambapo ni sawa na asilimia
16.
Akizungumza
jana Dar es Salaam katika mkutano uliohusisha viongozi wa Mkoa na Wilaya Dar es
Salaam kuhusu mwongozo wa kisera na mwongozo wa kutoa huduma kwa waathirika wa
ukatili wa kijinsia, Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadick alisema vitendo hivyo
vimekuwa vikiongezeka kila siku na kwamba vinatakiwa kukemewa.
Alisema
kutokana na utafiti wa Kitaifa wa Afya uliofanywa mwaka 2010, hali ya vitendo
vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto inaonekana kuwa mbaya hasa
katika Mkoa wa Dar es Salaam jambo ambalo linatakiwa kuwekewa mikakati sahihi
ili kutokomeza vitendo hivyo.
“Katika
utafiti wa Kitaifa uliofanywa mwaka 2010, umeonyesha kuwa kiwango cha ukatili
wa nyumbani kati ya wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 ni asilimia 45
ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam sababu kubwa inaweza kuwa mwingiliano wa watu
kitu ambacho ni vyema kikaangaliwa kwa undani ili kuondoa vitendo hivyo,”
alisema Sadick.
Alisema
ukatili huo unajumuisha ukatili wa kimwili asilimia 25, kingono asilimia saba
na asilimia 14 kwa aina zote mbili.
Ukatili wa wanawake wajawazito ni asilimia
tisa na asilimia 60 inaonyesha kwamba wanawake wajawazito hushurutishwa kufanya
ngono na wapenzi wao bila ridhaa yao.
“Matukio ya
ukatili wa kijinsia yanatofautiana kati ya mkoa na mkoa.
Mkoa wa Dar es Salaam
utafiti unaonyesha kuwa asilimia 46 ya wanawake na watoto wanafanyiwa vitendo
hivyo na asilimia 74 katika Mkoa wa Mara,” alisema Sadick.
Naye
Mkurugenzi wa Shirika la Usimamizi na Maendeleo ya Afya (MDH), Dk Guerino
Chalamilla alisema kila mtu anatakiwa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo
hivyo kwani havikubaliki katika jamii na kwamba ni kinyume na sheria.
Alisema MDH
kwa kushirikina na Serikali wameweka mikakati sahihi ya kuhakikisha wanatoa
elimu kwa watu wanaofanya vitendo hivyo ili kupunguza ukatili wa kijinsia
wanaofanyiwa wanawake na watoto.
“Kwa
kushirikina na Serikali tutahakikisha tunapiga vita na kuweka mikakati sahihi
ambayo inasaidia kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,”
alisema Dk Chalamilla.
Habari Na:Mwananchi






No comments:
Post a Comment